Lyrics
Mwenyewe anaona sawa ila mwambie mimi ananiumiza sana
Ni zaidi ya kupagawa siponi ugonjwa na nishamaliza dawa
Na ajue bado nipo ila hali yangu hohehahe, sina mabadiliko
Machozi mafuriko fundi wa jiko langu kaacha mawe, mpaka akalamba mwiko
(Toka alivyoniacha) Sina nyota wala mwezi
(Mwenzake nimekamatwa) Na homa ya mapenzi

Mwili watepeteka, sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari, naanza dhoofika

Bado ndo ndo ndo chururu nikijaza haikai kibaba
Na misongosongo msururu sita haikai saba
Mimi kitorondo ye kunguru mbao zangu hazimpi msaada
Makombe nishaoga dawa ka susuru huenda nikasahu labda
Kitandani mito ipo miwili ubavu wewe ubavu mimi
Pakata ndiko imewekwa shubiri nalikwepa nalala chini
Nimefuta picha tulizopiga chumbani ila bado zanisuta-suta zimebaki kichwani
Silali nastuka-stuka unaniita gizani chozi lalowesha shuka na sina wa kunifuta nani
(Toka alivyoniacha) Sina nyota wala mwezi
(Mwenzake nimekamatwa) Na homa ya mapenzi
(Toka alivyoniacha) Sina nyota wala mwezi
(Mwenzake nimekamatwa) Na homa ya mapenzi
Mwili watepeteka, sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari, naanza dhoofika
Mwili watepeteka, sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari, naanza dhoofika
(Toka alivyoniacha) Sina nyota wala mwezi
(Mwenzake nimekamatwa) Na homa ya mapenzi
(Toka alivyoniacha) Sina nyota wala mwezi
(Mwenzake nimekamatwa) Na homa ya mapenzi
Written by: Mbosso