Lyrics

[Verse 1]
Wasikuambie kwamba mimi eti sina lolote
Labda wakuambie sina ujanja juu yako
Wasikudanganye watakupa utakacho chochote
Wataitoa wapi furaha yako
[Verse 2]
Maana wabaya hawatoki mbali
Jirani yako we ndio anapenda usile
Hawatokubali kuona bendera ya penzi lako inapepea
Hawatokujali kipindi ambacho mawazo yanafanya usile
Watakutupia mbali
[Verse 3]
Si ulisema unataka gari na nimekubali kuenyeka mie
Tule mbegu na ugali kesho tutapata kipenzi nivumilie
Ukinitema itakuwa ni hatari utanipa na ajali kitanzi kuning'inia
Si tumetoka mbali
[Chorus]
Mazoea na ushakuwa maua (Moyo, moyo)
Wangu mimi unauendesha (Moyo, moyo)
Funga macho na masikio ziba (Moyo, moyo)
Usiwasikie, usiwaone pia (Moyo, moyo)
Umegota kwako, moyo wangu (Moyo, moyo)
Auu uuh (Moyo moyo) usiwaone pia
[Verse 4]
Kukosa majaribu moyo usije tia donda ukauchubua
Maumivu yani adhibu kisa upendo furaha kuichua
Kwenye kosa niadhibu nami mwanadamu siku ntakosea
Kukuacha sijaribu wapi niende nami kwako nishajifia
[Verse 5]
Ila usifanye kama fimbo, ufanane na tindo
Ukashindwa kujali maumivu yangu
[Verse 6]
Si ulisema unataka gari na nimekubali kuenyeka mie
Tule mbegu na ugali kesho tutapata kipenzi nivumilie
Ukinitema itakuwa ni hatari utanipa na ajali kitanzi kuning'inia
Si tumetoka mbali
[Chorus]
Mazoea na ushakuwa maua (Moyo, moyo)
Wangu mimi unauendesha (Moyo, moyo)
Funga macho na masikio ziba (Moyo, moyo)
Usiwasikie, usiwaone pia (Moyo, moyo)
Umegota kwako, moyo wangu (Moyo, moyo)
Auu uuh (Moyo moyo) oh moyo
[Outro]
Mooyo, heyy
Huu moyoo (Moyo, moyo)
Oh wangu mimi (Moyo, moyo)
Funga macho (Moyo, moyo)
Uuh baby (Moyo, moyo)
Funga macho
Heyy
Funga macho oh
Heyy, funga maa
Written by: Faustina Nandera Charles Mfinanga
instagramSharePathic_arrow_out