Lyrics
Hata kama penzi maji masafi niacheni nayanawa
Maana yamenifikaa, yamenifika hapaa
Ingawa ntakondaa, nimeridhia sawaa
Maana kila dakikaa, huwa kilionii
Kukikucha macho juu, nakesha kulilia penzi
Kama kinda alokosa mama eeh, mama eeh
Afu shida sio heshima tuu, hata wanaomuingia wengi
Mwenzenu kupenda nshakata tamaa eeh, tamaa eeh
We iache ikabaki kuwa historiaa, japo sio kiroho safi
Na ya nini kung'ang'ania biasharaa, tena yenye hasaraa
Na wala sisemi nitakuchukia, japo moyoo hautaki
Na ya nini kung'ang'ana ng'anang'ana iih
Inatosha, inatosha
Inatosha, inatosha
Ni kwamba moyo mashine, nina imani utapoa
Hii hali sio ya kudumu, nina imani utapoa
Ni kwamba tumeumbwa kusahau, nina imani ntasahau
Hii hali sio ya kudumu, ntakusahau
Kama kukupinga si ilishindikana, sawa sina chaguo
Maana Japo itanisumbua-sumbua, itaniumbua-umbua
Muchanga kwenye kitumbua-tumbua, kwenye kitumbua-tumbua
We acha ikabaki kuwa historiaa, japo sio kiroho safi
Na ya nini kung'ang'ania biasharaa, tena yenye hasaraa
Na wala sisemi nitakuchukia, japo moyoo hautaki
Na ya nini kung'ang'ana-ng'anang'ana iih
(Inatosha) Eeeh acha nipambane na hali yanguu
(Inatosha) Ahaa mapresha kupanda kushuka basii
(Inatosha) Mhh utaniua ehee
(Inatosha) Aah mmh utaniua mwenzako mie (Inatosha)
Written by: Marioo, Marioo Mwanga