Lyrics

Naumwa nina maradhi, nipelekeni Hospitalini
Mwenzenu Naumwa, moyo umekufa ganzi, nimechoka kunywa kwinini,
Nahisi ukichaa, nusu tahira uchizi, naona kinyabazongo
Niliyavagaa, rami nikaipiga mbizi
Ikanipasua ubongo
Angeniambia basi, tungeachana kizungu
Ningempa nafasi, kuliko kutupanga mafungu
Nisinge mgasi, japo ni ngumu machungu
Chanya na hasi, anapangaga Mungu
Kibatari kazidisha tambi, penzi limelipuka
Ye' ana-cheat haogopi dhambi
Anarukaruka, moyo kaupiga bambi
Umeshateuka, popote anaweka kambi
Kutwa anachepuka yani
Ndo wale-wale
Wanaokujaga kwa tafadhali nakupenda
Wale wale
Wakimaliza shida zao wanakwenda
Ndo wale-wale
Eti ooh nilipotoka nilitendwa
Wale-wale
Kumbe ni waongo
Nenda mwambie, mapenzi hayana jangiri yanaumiza
Tena mwambie, kuna walo matajiri wakalizwa
Usimfiche mwambie, mapenzi haya utabiri simiujiza
Fanya mwambie, mimi si wakwanza kuumizwa
Yaliwatesa vikongwe, tulisoma vitabuni
Nami amenipa mazonge, najikaza kisabuni
Sawa mimi nimnyonge, damu yangu yakunguni
Mi fungu la tatu kibonde, mwenzangu lake la kumi
Angeniambia basi, tungeachana kizungu
Ningempa nafasi, kuliko kutupanga mafungu
Nisinge mgasi, japo ningumu machungu
Chanya na hasi, yote anapangaga Mungu
Kibatari kazidisha tambi, penzi limelipuka
Ye ana-cheat haogopi zambi, anarukaruka
Moyo kaupiga bambi, umeshateuka
Popote anaweka kambi, kutwa anachepuka yani
Ndo wale-wale
Wanaokujaga kwa tafadhali nakupenda
Wale-wale
Wakimaliza shida zao wanakwenda
Ndo wale-wale
Eti ooh nilipotoka nilitendwa
Wale-wale
Kumbe ni waongo
Mwache afanye anachotaka
Anikomoi wala hanikomoi
Sistuki ata
Anikomoi wala hanikomoi
Sina hofu sina mashaka
Anikomoi wala hanikomoi
Anatapatapa
Written by: Lava Lava
instagramSharePathic_arrow_out