Lyrics

[Verse 1]
Vipeperushi vinasambaa eti natafutwa
Nimepotea wiki imekataa
Ndugu wamechachamaa, wananitafuta
Nimepotea mwezi umekata
[PreChorus]
Kazini sionekani, yupo wapi huyu
Simuni sipatikani, yupo wapi huyu
Baba kaniulizia, yupo wapi huyu
Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi
[Chorus]
Nimezama katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
Nimezama katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
[Verse 2]
Sio ya Andit Purre mwana Rajab mlomkuta Tanga
Sijafanywa msukule msipate tabu kumaliza waganga
Amenirudisha shule hesabu maumbo kupanga
Penzi la wasasambule lenye protini, vitamin na wanga
[Verse 3]
Aah! Ladha yake, si sukari
Ni vichenza na malimao
Mechi zake, huwa hatari
Ni chenga na mabao
[PreChorus]
Kazini sionekani, yupo wapi huyu
Simuni sipatikani, yupo wapi huyu
Baba kaniulizia, yupo wapi huyu
Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi
[Chorus]
Nimezama katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
Msinitafute, nimezama (Msihangaike katika kina kirefu)
Nipo salama, (Cha bahari ya mapenzi) salama, salama mimi
[Outro]
Nipo salama mimi, nipo salama mimi
Msinitafute, nipo salama mimi
Written by: Iraju Hamisi Mjege, Mbwana Yusuph Kilungi, Salmin Kasimu Maengo
instagramSharePathic_arrow_out