Lyrics
[Verse 1]
Una kila sababu ya kusimama kimaso-maso
Mungu kweli wa ajabu kanionyesha kwa yangu macho
Chukua zangu swahabu mi nibaki na dhambi zako
Unishikishe adabu mida ya kulala nitokwe jasho
[Verse 2]
Mi sijui kupigna mwili wangu wa mapenzi dear
Tusipende kugombana mi mwepesi kulialia
Si kujibanabana, raha ya penzi kujiachia
Wako mahututi mama, nimekufa nimejifia
[PreChorus]
Eeeh! Nalambishwa asali
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali
[Chorus]
Nimempata!
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata
[Verse 3]
Mi mTanzania wa halali, ila chembechembe za India
Mungu kaninyima ufahari, ila kwa huba najisifia
Sitakuhonga magari, ila mahaba utasanzia
Penzi kachumbari kwa ugali na pilipili ya kushagia, aah eeh!
[Verse 4]
Nikuite nani? Majina yote nishamaliza, aah eeh!
Wangu wa ubani umeweza kunituliza, aah eeh!
Mambo ya chumbani yaani nalala huku napulizwa, aah eeh!
Penzi zito tani napewa raha kupitiliza
[PreChorus]
Eeeh! Nalambishwa asali
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali
[Chorus]
(Nimempata) Nimempata mtaalamu nimempata
Nimempata! Nimempata mtaalamu nimempata
(Mtaalamu wa mapenzi) Nimempata mtaalamu nimempata
(Fundi wa mafundi kungwi) Nimempata mtaalamu nimempata
Kwa manake nimempata
Written by: Mbwana Yusuph Kilungi