Music Video

Harmonize - Nitaubeba (Official Video)
Watch Harmonize - Nitaubeba (Official Video) on YouTube

Featured In

Lyrics

[Verse 1]
Imagine uko jangwani umepotea
Mchana juani unatembea
Utokapo ni mbali, uendapo ni mbali
Mara ngamia mbebaji akatokea
Na kukushusha mzigo uliokuelemea
Upate afadhali pole na safari
[Verse 2]
And that's what you did to me
Yote tisa ila kumi
Umeonesha maana ya upendo
Si kwa maneno bali kwa vitendo
Umeridhika na nilicho nacho
Vya watu hutoleagi macho
Siku nikiwa sina twalala
Ooh baby twalala
[PreChorus]
Aah baby, before I close my eye
Mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie
We ndo pacha wangu mie
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena
Sikusikii ukilia, sikusikii ukisema
Niko busy na boo jamani nimeshasema
Niko busy na baby na msalaba wake
[Chorus]
Nitaubeba
Nitaubeba
Nitaubeba
Na nitafika nao kiume
Nitaubeba
(Iwe kwenye shida na raha)
Nitaubeba
(Ama kwenye shibe na njaa)
Nitaubeba
(La kwako ndo langu my darling)
Na nitafika nao kiume
[Verse 3]
Imagine hujifahamu umezimia
Umewekewa damu zinaingia
Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka
Mara dakitari wa zamu akaingia
Umepata fahamu unamwangalia
Machozi yanakuanguka unatamani funguka
[Verse 4]
And that's what you did to me
Yote tisa ila kumi
Unanifurahisha Kwenye tendo
Au unipe penzi la magendo
[PreChorus]
Aah baby, before I close my eye
Mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie
We ndo pacha wangu mie
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena
Sikusikii ukilia, sikusikii ukisema
Niko busy na boo jamani nimeshasema
Niko busy na baby na msalaba wake
[Chorus]
Nitaubeba
Nitaubeba
Nitaubeba
Na nitafika nao kiume
Nitaubeba
(Iwe kwenye shida na raha)
Nitaubeba
(Ama kwenye shibe na njaa)
Nitaubeba
(La kwako ndo langu my darling)
Na nitafika nao kiume
[Outro]
Iwe kwenye shida na raha
Ama kwenye shibe na njaa
La kwako ndo langu my darling
Written by: Arub Jahali
instagramSharePathic_arrow_out