Lyrics

Kiangazi, masika ukiichanganya, vyote vikashuka kwangu vitanielemea
Ntakosa pa kushika ntavavanya, wewe ndo mwandani wangu nliokuzoea
Mtunza vyangu visiri mwenye kunisitiri fundi mitambo, kinga yangu ya mwili usiyelipa bili kuchoma changu
Simtaki kafiri jangiri mwingi wa mambo, moyo akaukatilli, nikondeshwe mwili ajifanye Rambo
Si unajua dalili ya mvua mawingu, ikitaka kunyesha huwa yanatanda
Mami si unajua aah! Nimeumbwa na wivu, kidogo tu presha yashuka yapanda
Niahidi kama (Utatulia aah!), baby niahidi kama (Utatulia aah!)
Nisibaki nkashika tama (Utatulia aah!), baby niahidi kama (Utatulia aah!)
Wasiniibie cha ngama
Maneno yangu si Bibilia wala masaafu, tuseme usibadili
Jichunge kipenzi changu unanisikia, usicheze rafu, yatimie waliotabiri
Usijifanye Ronaldinho penzi utie mbwembwe utahaaribu, visokolokwinyo wakupitie denge kukujaribu
Kina Capachino wakakutia wenge kwa vizabibu, wakugongeshe mvinyo
Ukaota mapembe iwe aibu
Si unajua dalili ya mvua mawingu, ikitaka kunyesha huwa yanatanda
Mami si unajua aah! Nimeumbwa na wivu, kidogo tu presha yashuka yapanda
Niahidi kama (Utatulia aah!), baby niahidi kama (Utatulia aah!)
Nsibaki nkashika tama (Utatulia aah!), baby niahidi kama (Utatulia aah!), mmh wasiniibie cha ngama
Yani kama (Ukitulia-tulia), sitathubutu macho kupepesa (Ukitulia- tulia)
Ukinipa kiduchu nitatosheka (Kama ukitulia-tulia)
Sitofwata nguruchu niende teseka (Ukitulia-tulia), eeh eh, nami ntatulia
Written by: Lava Lava
instagramSharePathic_arrow_out