Credits
PERFORMING ARTISTS
Zuchu
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Zuchu
Songwriter
Nasibu Abdul Juma Issaack
Songwriter
Zuhura Othman Soud
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Lizer Classic
Producer
S2Kizzy
Producer
Lyrics
[Verse 1]
Mmh! Mh!
Lala, lala, lala
Mmh! Mh!
Lala, lala, lala (Ayo, Lizer)
Mmh! Mh!
Lala, lala, lala
Mmh! Mh! (Nusder)
[Verse 2]
Yani kwa sauti
Kasema deeka deeka
Na mimi najiachia
Kanipa shuruti
La kumteka-teka
Silaha kanigawia
Mbezi kimara
Hunipeleka-peleka
Mpaka mwisho hashuki, hashuki
Kiungo imara
Hunipenyeka-penyeka
Kwa ya nguvu mashuti, mashuti
[Verse 3]
Ooh, oh!
Kaniweka darasani
Kunifundisha vizuri
Mengi hayajulikani
Yataka kuyakariri
Kanichorea ramani
Kopa lenye nyingi siri
Jekundu nje na ndani
Rangi yake zingifuri
[Verse 4]
Raha upendwa raha (Mmhh! kupendwa raha)
Raha jamani raha (Naona raha)
Raha upendwa raha (Mmhh! kupendwa raha)
Raha jamani raha
[Verse 5]
Eti niende msituni
Zaraninge na matipwili nikamroge
Abadan, abadan
Penzi nichanjie mizaituni
Kwa vilinge na kuzikiri, linoge
Aah abadan, aah abadan, mmh
Vineno vya kisirani
Kafumwa na mwafulani
Mweupe mara kijani
Inawahusu nini?
Vipimo viso mizani
Kutwa kwenu midomoni
Tumewakaa vichwani
Mtumezee kwinini
[Verse 6]
Oohh
Ndege asili ya buga
Kufugwa hawezekani
Mithili ya kivuruga
Kaumbiwa kutamani
Atenda tafuta boga
Japo tama libandani
Ende tezi sina woga
Atarejea ngamani
[Verse 7]
Raha upendwa raha (Mmhh! kupendwa raha)
Raha jamani raha (Naona raha)
Raha kupendwa raha (Kupendwa raha)
Raha jamani raha
[Verse 8]
Ooh! Oh!
Ooh! Oh!
Ooh! Oh!
Written by: Nasibu Abdul Juma Issaack, Zuchu, Zuhura Othman Soud