Lyrics
[Verse 1]
Nimesadiki ya wahenga, penzi lina raha yake
Mzigo kwa tenga, kimfaacho mtu chake
Ndenge nimekatwa ngenga
Ah, umate-mate najinyenga nyenga (Mao mao, mao tate)
[Verse 2]
Huwaga sioni ninavyoipanda milima
Ulimi sikioni mwili wote wanizizima
Mwenzenu sioni macho mawili yote sina
Tunaanza jikoni mpaka varandani twalindima, yalah
[Chorus]
Yalah-yalah, yalah-yalah (Ooh)
Yalah-yalah, yalah-yalah
Penzi limenizidia (Yalah-yalah)
Ni kubwa (Yalah-yalah)
Nzito (Yalah-yalah, yalah, yalah)
[Verse 3]
Tungezaliwa zamani, ningesema penzi togwa
Tulinywe kibarazani tukitafuna maboga
Nimekipanda uani kibustani cha uyoga
Tukishiba biryani, baby, tule mboga-mboga
Sasa polisi wa nini? Nikikosa nikamate wewe
Mahakama ya nini? Nikikosa nihukumu wewe
Penzi chupa la balindi tuligide baby hadi tulewe
Vindege shorwe vya nini? Kifaranga unibebe weh mwewe
[PreChorus]
Huwaga sioni ninavyoipanda milima
Ulimi sikioni mwili wote wanizizima
Mwenzenu sioni macho mawili yote sina
Tunaanza jikoni mpaka varandani twalindima, yalah
[Chorus]
Yalah-yalah (Yalah-yalah), Yalah-yalah, (Yalah-yalah)
Yalah-yalah, yalah-yalah
Penzi limenizidia (Yalah-yalah)
Ni kubwa (Yalah-yalah)
Nzito (Yalah-yalah, yalah, yalah)
Written by: Mbwana Yusuph Kilungi