Lyrics

Kilicho nishawishi upole wako na heshima yako
Wazazi wangu wamekusifia sana kwa tabia yako
Sura yako ya upole, inanivutia
Shepu twiga mwenda pole, najivunia
Oh tupeane mapenzi iwachome (Ee), nakama namba waisome (Ee)
Hata tukigombana wasione (Ee), washike jembe wakalime (Ee)
Mapenzi mazuri ii wakutane wawili wanaopendana
Usizidishe washauri, watasababisha tuje kugombana
(Aae!) angalia shepu, (Aae!) Ka-Wema Sepetu (Aae!)
Angalia jicho, (Aae!) Hamissa Mobetto (Aae!)
Karangi kake, (Aae!) Elizabeth Michael (Aae!)
Yani we mrembo, (Aae!), walahi nachukua jiko, we ndio wangu wa milele
Nauza dagaa, ili ninunue motorcar nikuridhishe
Unanipa furaha, na nguvu ya kusaka chapaa nisikuangushe
Unanyota ya Adam na Hawa, ohoo tunavyopendana
Hata wakituchukia ni sawa, ohoo tuaminie mama
Wanaona umenipa dawa, ohoo wanaongea sana
Chunga usije kuota mbawa, ohoo ukaniachaga kilema
Katabiri pweza penzi litafika mbali
(Nacheka kiingereza) Ndio maana nacheza ya watu natupia mbali
(Mh Jamani) Katabiri pweza penzi litafika mbali, (Kwakweli hamtoweza) ndio maana nacheza ya watu natupia mbali
Basi baby nikumbatie mama (Aae!)
Angalia shepu, (Aae!) Ka-Wema Sepetu (Aae!)
Angalia jicho, (Aae!) Hamissa Mobetto (Aae!)
Karangi kake, (Aae!) Elizabeth Michael (Aae!)
Yani we mrembo, (Aae!), walahi nachukua jiko, we ndio wangu wa milele
Written by: Aslay
instagramSharePathic_arrow_out