Lyrics

Siku moja, moja ukipata nafasi tukumbukane
Nitalipa bodaboda achana na mwendo kasi usijibanebane
Ewe binti maringo sijui wanisikia, pendo lako nicheze bingo huenda nikajishindia
Mwenzako bado niko single, pendo limenichachia (Aah)
Uwe suka niwe tingo nyoyo iwe ya abiria
Nafsi unainyong'onyeza (Aah)
Nahisi la moyo shambulio (Aah)
Nifanye chipsi chombeza (Aah)
Japo unionje onje mwenzio (Aah)
Penzi linanilegeza
Sonona, Sonona
Eti lini utapata nafasi?
Sonona, Sonona
Beiby yoyo, nambie basi
Sonona, Sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi-wasi
Sonona, Sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi
Sonona, Sonona
Mwaga wino wa kalamu ya penzi langu, chimba shimo unizike kabla ya siku yangu
Hakuna asiyejua matatizo ya moyo ukipenda unanifanya mwanasesere kunichezesha
Mi muoga macho usoni sijashikwa na kwikwi kimasihara, sema niandae vipopkoni unyonye na vipipi vywa duara
Nafsi unainyong'onyeza (Aah)
Nahisi la moyo shambulio (Aah)
Mi nfanye chipsi chombeza (Aah)
Japo unionje onje mwenzio (Aah)
Penzi linanilegeza
Sonona, Sonona
Eti lini utapata nafasi?
Sonona, Sonona
Baby yoyo, nambie basi
Sonona, Sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi-wasi
Sonona, Sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi
Sonona, Sonona
Uje (Uje) Uje baby (Uje), uje Mombasa wakuone
Uje (Uje) Uje darling (Uje), uje Nairobi wakuone
Uje (Uje) Uje baby (Uje), uje Dar es Salaam wakuone
Uje, uje baby, 001 akuone
Written by: Mbosso
instagramSharePathic_arrow_out