Lyrics

Naogopa nikiwambia watu sijui wataniona vipi!
Naogopa kuyasema yote acha tu ninyamaze kimya (Hey, hey, hey)
Naogopa kuwaambia watu wanaanza kunisengenya
Nina maswali mengi miguuni pako
Kwa nini Mungu umekuwa kama vile huoni
Pesa sina lakini umeacha niuguee
Namtegemea lakini umemwacha aondoke
Kwa nini Mungu umenyamaza aa
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali naa mlima ni mkali umenyamaza!
Maumivu ni makali na vita ni vikali, nimevumumilia nimeshindwa sema kitu
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali naa mlima ni mkali umenyamaza!
Maumivu ni makali na vita ni vikali, nimevumumilia nimeshindwa sema kitu
Ona kwa yule ulitenda juzi na leo tena, kuna ugumu gani kwangu Baba sema basi
Mimi binadamu nakosa majibu sema Baba, nakuamini sana Baba yangu usiniache
Kuna shida gani! Imekuaje! Hata usiseme, kama ni kosa naomba unisamehe, turekebishe naomba unisamehe
Nitateta nawe sitakata tamaa wakuamua yangu bado ni wewe, na kuamini Mungu bado ni wewe
Naogopa, uko kimya kuna nini Mungu sema neno usikae kimya nisije kufuru Mungu
Kama siku zangu za kuishi duniani bado zipo oo naomba sasa Baba umalize, umalizane na shida zanguu
Mambo mengii nimeomba kwako umejibu hili hujajibu, Mungu wangu bado nasubiri kwako
Jibu basi watu wakuone wewe, watu wakuone Baba, bado nasubiri kwaako
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali naa mlima ni mkali umenyamaza!
Maumivu ni makali na vita ni vikali, nimevumumilia nimeshindwa sema kitu
Maumivu ni makali na vita ni vikali, nimevumumilia nimeshindwa sema kitu
Written by: Emmanuel Zabron Philipo, Hamis Joseph Bukulu, Marco Joseph Bukulu, Victoria Zabron Philipo
instagramSharePathic_arrow_out