Lyrics

[Verse 1]
Kuna wakati ukinyamaza unakosa baraka
Maana Yesu anataka useme ili atatue shida zako
Mimi sitaki tena mimi kunyamaza nitazitaja tajaa
Shida zangu zote nitamwambia yesu ili azitatue
[Refrain]
Baraka (Nitasema) nibariki (Nitasema)
Na shida (Nitasema) niugue (Nitasema)
Nitasema yote kwako yesu wangu
Labda mimi ndiyo batimayo wako leo
[Verse 2]
Sisikilizi la mtu, sibadili mtazamo
Hata wanadamu wanizibe mdomo wakidhani sisitahili mimi ni mdhambi
[PreChorus]
Yanini niuumie moyo hata usijali (Wakati Yesu upo)
Nichekwe nidharauliwe na kusimangwa (Naamini we upo)
Niishi maisha magumu hata usijali (Wakati yesu upo)
Nikose ka gari na nyumba Maisha mazuri (Naamini we upo)
[Chorus]
Nita drive, nifagie na kanyumba kangu
Niende banki, nihesabu na vi pesa vyangu
Nita drive, nifagie na kanyumba kangu
Niende banki, nihesabu na vi pesa vyangu
[Verse 3]
Majereha unapitia moyo waumia umenyamaza
kimywa kimywa na hausemi chozi shavuni ni kama chakula
Wajishauri umweleze nani wa kuweza kusitisha
shida zote maumivu ya dunia hapa hapa chini ya jua
[Verse 4]
Sina pesa (Nitasema) chakula (Nitasema)
Mawazo (Nitasema) kuonewa (Nitasema)
Nitasema yote yote kwako Yesu wangu labda mimi ndiyo zamu zamu yangu leo
[Verse 5]
Nakuamini ni wewe wakuamua ni wewe
Hata wanadamu watadhani Baba umeniacha
Kumbe ni jaribu la mda tu
[PreChorus]
Yanini niuumie moyo hata usijali (Wakati Yesu upo)
Nichekwe nidharauliwe na kusimangwa (Naamini we upo)
Niishi maisha magumu hata usijali (Wakati yesu upo)
Nikose ka gari na nyumba Maisha mazuri (Naamini we upo)
[Chorus]
Nita drive, nifagie na kanyumba kangu
Niende banki, nihesabu na vi pesa vyangu
Nita drive, nifagie na kanyumba kangu
Niende banki, nihesabu na vi pesa vyangu
Written by: JAPHET ZABRON PHILIP
instagramSharePathic_arrow_out