Credits
PERFORMING ARTISTS
Zabron Singers
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
JAPHET ZABRON PHILIP
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Joshua Katumbo
Producer
Lyrics
[Chorus]
Hili limeniliza saana hili limeniumiza sana
Awamu hii nimeumia sana Mungu wangu nisaidie
Mbona umeniacha sana katika hili nimeumia saana
Nakiri nakuhitaji sana Mungu wangu nisaidie
[Verse 1]
Ungeniuliza nisingekubali mimi mpendwa wangu nimwachee aende
Rafiki yangu kipenzi aende Mungu hapana kwangu si sawaa
Ile mipango tulipanga imezima kwako ni sawa ila nabaki pekee yangu
Nitafanyaje nimeachwa pekee yangu Mungu hapana kwangu si sawa
[Verse 2]
Ila naelewa Mungu kazi yako haina kosa
Nakushukuru kwa yote mapenzi yako yatimizwe
[Chorus]
Hili limeniliza saana hili limeniumiza sana
Awamu hii nimeumia sana Mungu wangu nisaidie
Mbona umeniacha sana Katika hili nimeumia sana
Nakiri nakuhitaji sana Mungu wangu nisaidie
[Verse 3]
Japo nawaza nafarijika Bwana kwamba kunayo siku tutakutana naye
Ilee asubuhi njema uliyoiweka pale kwa watu wanaokuamini Yesu
Nitie nguvu baba nimechoka moyo unauma nimechoka
Nisaidie Baba nimechoka pekee yangu mimi siwezi
[Verse 4]
Tufundishe Mungu wetu kuhesabu siku zetu
Japo dhoruba na shida tusichoke kukutumikia
[Chorus]
Hili limeniliza saana hili limeniumiza sana
Awamu hii nimeumia sana Mungu wangu nisaidie
Mbona umeniacha sana katika hili nimeumia saana
Nakiri nakuhitaji sana Mungu wangu nisaidie
[Refrain]
Mtu wa watu huyuu mwenye upendo huyuu
Mpatanishi huyuu kaenda vipi tena
Mtu wa watu huyuu mwenye upendo huyuu
Mpatanishi huyuu kaenda vipi tena
Written by: JAPHET ZABRON PHILIP