Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Zabron Singers
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Zabron Singers
Songwriter
JAPHET ZABRON PHILIP
Songwriter
Marco Joseph Bukulu
Songwriter
Lyrics
[Verse 1]
Ninaye rafki kipenzi, kipenzi namwita mama
Ana pacha wake yeye ninamwita daddy
Hawa ni wazazi wa mimi, na leo nina wimbo wao
Tuseme mazuri mengi walotufanyia
[Verse 2]
Nikianza na mama we ndo wangu superwoman (Superwoman)
Unajua mengi juu ya mi mwanao mama
Kwanza nilikusumbua, utoto ni vita-vita
Na vistick nilichezea, lengo unifunze tabia njema
[Verse 3]
Mama haa, tumboni ulinibeba
Na uvumilivu mimi ukanilea
Miezi tisa tumboni mwa mama
Shida mateso yote nilivumilia
[Verse 4]
Nilipozaliwa mimi ulinivisha na kuninywesha
Nilipokuwa mdogo ulihakikisha niko salama
Nakupenda mama, haa
Asante mama, hee
[Verse 5]
Hata siku ya birthday yako ikifka
Nitakuimbia, happy birthday mummy
Happy birthday mummy
I love you mama
[Verse 6]
Namzungumzia mama, mama, mama yetu mama
Mi mwanao ninakupenda, mama nani kama mama
[Chorus]
I love you mummy (Mama)
I pray for you mummy (Wangu mama)
Nakupenda mama (Mama)
I pray for you mama (Wangu mama)
[Verse 7]
Baba ulihangaika baba
Upate chochote wanao tule
Na nguo tuvae, na shule twende baba, tussore, twende
Nakumbuka na ule usia, kusali kuomba tushike
Niwe mtu mwema kwa Mungu na watu niwe mtu wa watu
[Verse 8]
I love, I love you
I love you, I love you daddy
Namzungumzia baba, baba, baba yetu baba
Mi mwanao nakupenda
Baba, baba yetu baba
[Verse 9]
I love you daddy
I pray for you daddy
I love you daddy
I pray for you daddy, daddy
[Verse 10]
Nitakuja nyumbani nichukue baraka
Maisha yangu yapendeze mama
Umwambie na baba, nampendaga sana
Anipe neno la baraka pia
[Verse 11]
Kuna muda namuomba Mungu awazidishie
Uzima maisha mazuri nije niwatunze
Muone matunda ya mi mwanenu
Muone na niwafurahishe, I love you
[Chorus]
I love you daddy (Baba)
I pray for you daddy (Wangu baba)
Nakupenda wangu baba (Baba)
I pray for you daddy (Wangu baba)
[Verse 12]
Amri ya tano na ya Mungu
Waheshimu baba na mama yako
Na siku zako zije kuwa nyingi
Zipate kuwa nyingi, zipate kuwa nyingi
Asanteni wazazi nawapenda
Hakika nyinyi ndio kila kitu kwangu
Hata baraka zangu chanzo ninyi
Nawaombea mema, nawaombea mema
[Outro]
I love you, I love you
I love you mummy
Daddy, daddy-daddy
Mummy, mummy-mummy
Daddy mi mwanenu nawaombea kwa Mola
Written by: JAPHET ZABRON PHILIP, Marco Joseph Bukulu, Zabron Singers