Lyrics

Sijui hata nifanyeje, sijui hata nifanye nini me, maana hata siamini
Nilikula kiapo nikungoje ila bado haiingi akilini, maana nishakula ya mini yawe
Kwa mashogazo ulichota mafumbo, ngoja-ngoja inaniumiza tumbo, masikini umeshafata mkumbo, yaani umesepa
Umeziacha zimejaza na rundoo, na una ponda yangu fupi myundo, eti unaning'ong'a, tajiri wa uvundo ndio chanzo umeniteka
Na naimani nitajijengea nisikuwaze kwa ubaya, kwa ubaya, maana before nlitimia, leo uwe mfano wa bandama umebanduka
Labda yangu nyota imefifia wamekuteka we ah, we ah, simanzi imenielemea shilingi imepinduka
Kama usiporudi (Nitachelewaa), oh oh (Kupona nitachelewa), ah nitachelewam mama (Nitachelewa), hmm-hmm (Kupona nitachelewa)
Kupona maradhi ya moyo (Nitachelewaa), yeah (Kupona nitachelewa)
Kama sio wewe nani tena (Nitachelewaa), oh no (Kupona nitachelewa), nitachelewa mama
Mi najaribu kujisahaulisha ila moyo unagoma, unagoma, hasa nikikumba zako methali na nahau
Japo unanionyesha dharau, moyo hautaki komaa, kukoma, mwingine sitaki penda na usidhani ka nitakusahau
Maana vita penzi lako ntapiga na nikiamini utarudi we changama, maana siko sawa ujue, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
Wanaogombana siku zote ndio wananopatana ama unapenda mi ninavolalama
Sijui nilipokosa ujue, na malengo ujue, mimi najua wewe langu fungu
Na naimani nitajijenge, nisikuwaze kwa ubaya, kwa ubaya, maana before nlitimia, leo uwe mfano wa bandama umebanduka
Labda yangu nyota imefifia wamekuteka we ah, we ah, simanzi imenielemea shilingi imepinduka
Kama usiporudi (Nitachelewaa), oh-oh (Kupona nitachelewa), ah nitachelewam mama (Nitachelewa), hmm-hmm (Kupona nitachelewa)
Kupona maradhi ya moyo (Nitachelewaa), yeah (Kupona Nitachelewa)
Kama sio wewe nani tena (Nitachelewaa), oh no (Kupona nitachelewa), nitachelewa mama
Written by: Ibrahimu A N
instagramSharePathic_arrow_out