Credits

PERFORMING ARTISTS
Chidi Benz
Chidi Benz
Vocals
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Chidi Benz
Chidi Benz
Songwriter
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Bob Junior
Bob Junior
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Me niliambiwa mapenzi ni kama bahari
Ukishazama ndo basi umepotea
Kumbe mwenzangu alikuwa na tanari
Badala ya kuzama me kwangu akaelea
[Verse 2]
Akawa ananidanganya
Nikiwa nadhani ananipenda sana
Mikwanja nikamwaga mama
Japo sio kivile ila kwangu ya maana
[Verse 3]
Wakawa ananidanganya
Nikiwa nadhani ananipenda sana
Mbona mifedha nikamwaga mama
Japo sio kivile ila kwangu ya maana
[Verse 4]
Wakaja wajinga wakamchukua
Wakamhonga honga mwisho wakamnunua
Wajinga wakamchukua
Wakamhonga honga mwisho wakamnunua (Ayayayayaa)
[Chorus]
Usinione nalia (Ra), usinione nalia (Ra), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (Ra), nalia (Ra), nalia na mengi
(Uuh) Jamani nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
[Verse 5]
Najua alimaanisha kuwa simfai ila lakini angesema
Kuliko alichofanya me akantoa nishai akanimeza akanitema
Nyie mapenzi yanauma vibaya, vibaya, vibaya
Mmh mapenzi yanauma vibaya, vibaya, vibaya
[Verse 6]
Ile ghafla safari ndio inanifanya mi usingizi sipati
Huwa nakumbuka mbali
Hasa nikisikia harufu yake ya marashi
[Verse 7]
Me kwa uchungu nilivyoumia
Nikaandika hili songi la mwanduku nalia
Na vocal nikaingiza kwa hisia
Naimani iko siku nyimbo itamfikia
[Verse 8]
Me kwa uchungu nilivyoumia mie
Nikaandika songi la mwanduku nalia
Na vocal nikaingiza kwa hisia
Naimani ipo siku nyimbo itamfikia (Ayayayaa)
[Chorus]
Usinione nalia (Ra), usinione nalia (Ra), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (Ra), nalia (Ra), nalia na mengi
(Uuuh) jamani nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
[Verse 9]
Usione nakosa raha mama nalalama kwako mara kadhaa
We ni msaada kwenye tuta so ukichomoka balaa
Sijiwezi kwangu giza naweza kimbiza na hii taa
Na hilo unajua inavyoumiza ushashuhudia mara kadhaa
[Verse 10]
We ndo urithi wakung'ang'anie ninung'unike nilie
Njia yetu moja niache nipite suka usinibanie
Kwa mahaba ya kinyamwezi na swaga zako juu
Na miguu napata picha kitandani kungfu
[Verse 11]
Uko juu ukipita lazima wasome namba
We ndo kibri fimbo kiboko ya midomo mamba
Huu ndo mfano hata unajua neno pamba sifa yake
Kwa kitambo ntakulinda kama mkinga mwenye shamba
[Verse 12]
Mikogo kila leo ntajigamba nusu soldier nusu mpweke
Kisela piga teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke, eeh bounce
[Chorus]
Usinione nalia (Ra), usinione nalia (Ra), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (Ra), nalia (Ra), nalia na mengi
(Uuh) jamani nalia (Ra), nalia (Ra), sababu ya mapenzi
Written by: Chidi Benz, Diamond Platnumz
instagramSharePathic_arrow_out