Music Video

Ibraah - Mapenzi (Official Music Video)
Watch Ibraah - Mapenzi (Official Music Video) on YouTube

Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ibraah
Ibraah
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ibraah
Ibraah
Songwriter

Lyrics

Amini unayempenda naye ana wake anayempenda pia, na siku zinakwenda
Na hata yule anayempenda naye ana wake anayemwita dear, haya mapenzi mwana kwenda
No ooh ni yale yale mapenzi yaliyowatesa mabibi na mababu hadi leo, mie mwenzenu siyawezi ni bora uyashuhudie kwa mwenzio ama kwa video
Usione mtu ataliaga ukadhani ni utoto, mapenzi yana vingi vituko nyingi changamoto
Oona, ukimpata anaye kuthamini na tulia na utunze yake heshimaa ujue ndo kashazama kwa kina weewe
Vipo vya kuvumilia (Lakini sio mapenzi), mapenzi yanaumiza (Mi' ndio maana siyawezi)
Vipo vya kuvumilia (Lakini sio mapenzi), mapenzi yanaumiza aah mapenzi
Nawe penda unapopenda unapo amini kwamba amani ya moyo wako ipo, na ukikosa unachopenda utapagawa bure hata ufanye matambiko
Nana hata ukimpenda kweli hawezi jua sababu ni siri ya moyo wako, hata kama akifeli atapuuzia ili uteseke tu peke yako
Ngoswe kitovu cha uzembe ukipenda huoni na unayempenda hajui hatambui kama yeye ndo yako mboni
Hata akisema amechoka anataka mwachane wewe zidi kumpenda tuu ivyo-ivyo maana mapenzi hayana mwenyewe
Unaweza ukaondoka ukaenda kupenda pengine napo ukakuta ndivyo sivyo ukajihisi una mkosi weewe
Ukimpata anayekuthamini na tulia na utunze yake heshimaa ujue ndo kashazama kwa kina weewe
Vipo vya kuvumilia (Lakini sio mapenzi), mapenzi yanaumiza (Mi ndio maana siyawezi)
Vipo vya kuvumilia (Lakini sio mapenzi), mapenzi yanaumiza aah mapenzi
Written by: Ibraah, Ibrahim Abdallah Nampunga
instagramSharePathic_arrow_out