Lyrics

[Verse 1]
Kuidhulumu nafsi sitaki
Penzi la ukakasi sitaki
Mi najua mna upendo wa dhati
Sa kwanini niingie kati
[Verse 2]
Mioyo yenu ipeni nafasi
Muinywe kwa uhuru sharubati
Penzi lisiwe la hisabati
Mpaka muushangaze umati yooh
[PreChorus]
Apendapo maulana basi na mimi
Nipate wa kushibana
Halafu nyinyi cheki mnavyopendana
Si kwa matendo, kwa ishara tunaona
[Chorus]
Aah penzi lenu liwe kisima cha upendo
Ololoo maah liwe la shine like a diamond
Wanga wakae mbali, liwe kisima cha upendo
Ololoo maah liwe la shine like a diamond
Diamond
[Verse 3]
Mapenzi sio ya kulazimishana
Wanaopendana kuwaachanisha ni laana
Angalia macho yao, mazuri yanavyofanana
Na watu wasiopendana utawapata wakishindana
[Verse 4]
Yapo kama maua, kuna muda yatachanua
Mtashindwa kutambua, wapi linapiga jua
Mapenzi kitumbua, mchanga msije tia
Waacheni wamekua, sisi tuombe dua aah
[PreChorus]
Apendapo Maulana basi na mimi
Nipate wa kushibana
Halafu nyinyi cheki mnavyopendana
Si kwa matendo kwa ishara tunaona
[Chorus]
Aah penzi lenu liwe kisima cha upendo
Ololoo maah liwe la shine like a diamond
Wanga wakae mbali, liwe kisima cha upendo
Ololoo maah liwe la shine like a diamond
Diamond
[Outro]
Diamond
Diamond
Diamond
Written by: Sharif Saidi Juma
instagramSharePathic_arrow_out