Top Songs By Stamina Shorwebwenzi
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Stamina Shorwebwenzi
Performer
Bonventure Eliuter
Rap
COMPOSITION & LYRICS
Boniface Kabogo
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Bea
Producer
Lyrics
Unaposkia neno ndoa (Ndoa), ujue noma, kabla kuongea chochote, naomba kwanza kusonya
Aliyenifundisha mapenzi hakuniambia kuhusu kuoa, alinionyesha staili za tendo ila sio maisha ya ndoa
Aliyesema ndoa ndoano hivi huyu mjinga ni nani? Kafanya nivue samaki kwenye bahari yenye tsunami
Nikiziona picha za harusi najiskia vibaya, namuonea huruma padri pamoja na waimba choir
Yale mafunzo ya katekista eti yamepotea mazima, sadaka misa ya ndoa bora mngewapa watoto yatima
Pole wasimamizi wa ndoa kwa ujinga mliosimamia, mngesimamia ukucha mngekuza hata familia
Kama ni pete nisharudisha kwa sonara, tayari nishavuta mpunga nimerudisha nusu hasara
Kabla kuingia ndoani anakuwa kondoo usiyemjua, ila ukimweka ndani nyani anakuachia mabua
Marafiki, mashemeji ndio wanafiki nakuambia, wanaweza kufanya ulewe bila hata kukupa bia
Sasa ile suti (Ilifanya ya nini?), na mchango (Nilichangisha ya nini?)
Na wale ndugu (Niliwaita wa nini?), na kile kiapo (Niliapa kwa nini?)
Naubembeleza upepo, usizime kibatari (Iye, iye, iye)
Kichwani mwangu hayupo, moyoni niko shwari (Iye, iye, iye)
Ona hajaacha pengo mwambie (Asiwaze), huko aliko atulie (Asiwaze)
Kama amepoteza lengo mwambie (Asiwaze), huko aliko atulie (Asiwaze)
Mwambieni yule dogo aliyeichezea club ya Simba, kutembea na mke wangu asijione kama ameshinda
Mi samaki, mapenzi yangu yana chombo, kaka yake nishakula so ruksa kutoa vyombo
Hata posa nililotoa mwambieni aingize vikoba, ila atakaye muoa ampe mtaji wa bodaboda
Ama kweli hii dunia ina mambo mengi, na ndoa ni kama boti haiwezi kupaki stendi
Hichi cheti cha ndoa nimebaki nacho kwa nini? Siwezi kuombea kazi hakina mchongo apa mjini
Hata Biblia imeandika wanawake tuishi nao kwa akili, kwao sikumficha kitu ulimpa hadi sehemu za siri
Akiskia nimekufa mwambieni asilie sana, aite rafiki wafurahi wachome nyama
Nitazikwa na ndugu, rafiki na mafans kibao, mkimuona msibane nitafufuka nimzabe vibao
Unaweza kumpakia mkongo mkeo na usimfikishe, alafu anayempakia mkorogo ndio akamfanya amridhishe
Ndoa ndoana anayebisha aniulize mimi, nishawahi kuwa na mahusiano ambayo sijui yanahusiana na nini
Na ile keki (Nilikata ya nini?), na mahari (Nililipa kwa nini?)
Na yule mshenga (Nilimtuma wa nini?), we si uliapa tena ukala yamini
Naubembeleza upepo, usizime kibatalii (Iye, iye, iye)
Kichwani mwangu hayupo, moyoni niko shwari (Iye, iye, iye)
Ona hajaacha pengo mwambie (Asiwaze), huko aliko atulie (Asiwaze)
Amepoteza lengo mwambie (Asiwaze), huko aliko atulie (Asiwaze)
Asiwaze, asiwaze, asiwaze
Written by: Boniface Kabogo