Top Songs By Stamina Shorwebwenzi
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Stamina Shorwebwenzi
Performer
COMPOSITION & LYRICS
BONVENTURE ELIUTER KABOGO
Songwriter
PAUL THIMOS MWASILE
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
PAUL THIMOS MWASILE
Producer
Independent artist
Producer
TML
Producer
Lyrics
Intro
Yeeeeyehh/
Aaaah/
Toa ndugu/
Anakuona/
Verse 1
Eeh!kama nina nguvu ya kutafuta siwezi ita mtu Tajiri/
Tajiri sio kipaji ni kazi nguvu na akili/
Tatizo tukipata pesa tunapoteza marafiki/
Harafu tunapata wapambe ambao hatukuwa nao kwenye dhiki/
Neno la ufahamu ni lile neno lenye elimu/
Ila neno lenye utamu ni lile lililotiwa ndimu/
Japo wengi hawafahamu tofauti ya hamu na stimu/
Kama ilivyo tofauti ya maarifa na elimu/
Kipindi unamtongoza demu ili uonekane mjanja/
Mi namtongoza dalali ili nipate kiwanja/
Harafu sasa,ukipaka mkongo umkomoe mchumba/
Mwezako niko site ndio naipaka rangi nyumba/
Eeh!
Tusibishane kuhusu hili kuna vichwa viwili/
Ila cha chini hakifikiri/
Mwanume aliyevaa vikuku aliyetoga masikio na pua/
Huyo mwanaume sie hatuhusu sio mwanaume tunaemjua/
Maskini wenge tuna ndoto za utajiri kichizi/
Hazitimii sababu tunastuka katikati ya usingizi /
Hatujakuzwa kuamshwa na alarm ili tuamke/
Tunaamshwagwa na shida Tuache shuka tukatafute/
Chorus
Toa ndugu ,toaaaa(toa ndugu)
Toa ulicho nacho (ulicho nacho)
Bwana anakuona(anakuona)
Mpaka moyoni mwako x2
Verse 2
Acha nikwambie/
Kuna urithi wa aina mbili/
Kuna urithi wa mali na ule urithi wa akili/
Urithi wa mali,utakupa mali za utajili/
Ila urithi wa akili unaweza usikupe akili za dili/
Na kwenye Maisha/
Maisha hayaishi sababu yako
Ila wewe ndio unasababu ya kuishi kivyako /
So kabla ya kuvuta ganja hakikisha unavuta pumzi/
Maana pesa ni mwanamke ambae abaki kama umtunzi/
Na kwenye ukoo sina ndugu yeyote Tajiri/
Na kama yupo basi lazima awe mbahiri/
Mungu anables adoado najikongoja/
Na ghetto nikiishiwa gesi nawasha data naunga mboga/
Mama angu pekee ndiyo mwanamke nae mwamini/
Japo nae alirubuniwa ndiyo nikapatikana mimi/
Peace kwa wanawake wote kima cha chini na juu/
Nawapa mimba za fikra msimeze p2/
Mambo madogodogo hayo nitawapa haina kwele/
Siwezi kuwapa nyumba labda nyumba za milele/
Na kuhusu kupush mtapush mkipata mimba/
Kwa hiyo ni udhushi nikisema mtapush ndinga/
Chorus
Toa ndugu ,toaaaa(toa ndugu)
Toa ulicho nacho (ulicho nacho)
Bwana anakuona(anakuona)
Mpaka moyoni mwako x2
Hook
Usifanye moyo wako kuwa mgumuu wewe…..
Toa ulicho nacho huende bwana anakuona….
Written by: BONVENTURE ELIUTER KABOGO, PAUL THIMOS MWASILE