Lyrics

[Verse 1]
Mola kamuumba hana mfano wee
Mzuri wa sura na roho na njema tabia iyaaa
Unyagoni kafundwa kwa makungwi somo wee
Mahaba Kayajaza ndoo yananimwagikia iyaa
[Verse 2]
Natamani nimtaje hata jina
Ila naficha, naficha naifanya siri yangu
Kina fulani wale wakusigina mkaleta mapivcha, mapicha
Akatoroka ndege wangu
[PreChorus]
Si mrefu si mufupi (Ah eh)
Si mweupe si mweusi (Ah eh)
Rangi yake ni ya katikati
Kasema kwangu hafurukuti (Ah eh)
Kwengine anaogopa nuksi (Ah eh)
Mi ni wake milele haniachi ndo maana
[PreChorus]
Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja (Nani)
Amenifika kwa roho
Makopakopa (Kopa)
Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja (Nani)
Ila kumtaja ooh naogopa ogopa
Kwa jina namuhifadhi
[Chorus]
Desh-desh, desh-desh (Msije kuninyakulia)
Desh-desh, deesh (Kipenzi changu jamani)
Desh-desh, desh-desh (Mkaja kuniharibia)
Desh-desh, deesh (Penzi likawa mashakani)
[Chorus]
Nananaa! Nna, nna!
Nananaaa! Nna, nna!
Nananaa! Nna, nna!
[Verse 3]
Najua, najua roho zinawauma
Hampendi kuona mwenzenu na nawiri
Najua mwenzenu najua, mwakesha kujituma
Kutwa kwa masangoma, yangu kuyatabiri
[Verse 4]
Mlosema nimeachika hainifiki mikosi (Mola ndo mpaji)
Nyongo mtazitapika mchomwe jua la utosi (Kesheni kunijaji)
Mwenzenu kila kukicha kabla kupewa misosi (Masaji masaji)
Tunavyowakasirisha yani hata tukiposti (Hataki nimtagi)
[Verse 5]
Enhee si mtu wa magazeti wala page za udaku
Ilo mkae mjue hataki-taki eenhe
Mambo yake siri nyeti poleni washakunaku
Wala msijisumbue kumsachi-sachi
[PreChorus]
Nampenda Mpenda (Nani), kijana mmoja (Nani)
Amenifika kwa roho makopa-kopa (Kopa)
Nampenda mpenda (Nani), kijana mmoja (Nani)
Ila kumtaja ooh naogopa-ogopa
Kwa jina namuhifadhi
[Chorus]
Desh-desh, desh-desh (Msije kuninyakulia)
Desh-desh, deesh (Kipenzi changu jamani)
Desh-desh, desh-desh (Mkaja kuniharibia)
Desh-desh, deesh (Penzi likawa mashakani)
[Chorus]
Nananaa! Nna, nna!
Nananaaa! Nna, nna!
Nananaa! Nna, nna!
Written by: Lava Lava
instagramSharePathic_arrow_out