Music Video

Credits

PERFORMING ARTISTS
Lava Lava
Lava Lava
Lead Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Lava Lava
Lava Lava
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Lizer Classic
Lizer Classic
Producer
Manster Madness
Manster Madness
Producer

Lyrics

Una rangi ya chotara manga-manga asili ya kizanzi bari
Chocolate color mixer mtanga tanga unang'ara ng'aring'ari
Ngozi laini kachori sambusa bagia
Upo kama mdoli yaani kama wabandia
Ukitembea koko (Koko) uko nyuma baikoko (Koko) mzigo sio wa buku jero
Sotojo la bokoboko (Koko) laini nyanya ya kopo (Kopo) yaani bunyero-bunyero
Achana na kina Gigi hawana lolote, watazusha nawajigijigi penzi watie tope
Nikupeleke kwa bibi Tifah ma Dangote, uvae shela wigi utapata kwa Aristote
Habibi (Habibi) Nurul'ayn kipenda roho (Habibi) nyonga mkalia ini
(Habibi) Nurul'ayn kipenda roho (Habibi) nyonga mkalia ini
Penzi lisiwe dibaji zidisha utamu tende, mahaba yawe full chaji tukomeshe fisadi viwembe
Nikandekande massage wabaki kupiga vijembe, weka hiriki magadi ongeza na peremende
(Ah haa) Mchunge shetwani mama twende pole-pole, (Ah haa) kuna Esma Khan na kina Juma Lokole
(Ah haa) Wasikupande kichwani wakazua mambo uchocholee, (Ah haa) iwe aibu mtaani Insta michambo wanichore
Achana na kina Gigi hawana lolote, watazusha nawajigijigi penzi watie tope
Nikupeleke kwa bibi Tifah ma Dangote, uvae shela wigi utapata kwa Aristote
Habibi (Habibi) Nurul'ayn kipenda roho (Habibi) nyonga mkalia ini
(Habibi) Nurul'ayn kipenda roho (Habibi) nyonga mkalia ini
Usije kughairi ghairi, (Mi mwingine sina) usije kughairi ghairi (Penzi likachina)
Usije kughairi ghairi, (Ukanitosa mazima), Usije kughairi ghairi, (Nuru ikazima)
Written by: Lava Lava
instagramSharePathic_arrow_out