Top Songs By Ambwene Mwasongwe
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Thimos Chelula
Producer
Lyrics
[Chorus]
Pita, pita, pita mbele yangu pita
Pita, pita, pita mbele yangu pita
Aah, aah, aah, aah
Aah, aah, aah, aah
[Verse 1]
Ni kweli nimepanga mambo mengi kufanya
Lakini usalama wangu umebaki kwako mwenyewe
Ndio maana leo nimekuja kupiga magoti mbele zako
Ninaomba nisaidie uende mbele yangu
[Verse 2]
Macho yangu hayaoni nini kiko mbele
Natumaini wewe wewe umeona
[Verse 3]
Tangulia mbele yangu Bwana kanyooshe mapito
Siwezi kwa ufahamu wangu nataka leo nishinde
[Chorus]
Kama ukienda mbele yangu
Hakuna jambo gumu nitashindwa
Nitajiachia kama tai
Nikijua wewe uko mbele
[Chorus]
Kama ukienda mbele yangu
Hakuna jambo gumu nitashindwa
Nitajiachia kama tai
Nikijua wewe uko mbele
[Chorus]
Pita, pita, pita mbele yangu pita
Pita, pita, pita mbele yangu pita
[Verse 4]
Ni kweli nimepanga mambo mengi kufanya
Lakini usalama wangu umebaki kwako mwenyewe
[Verse 5]
Nataka kuwa shujaa Bwana nisaidie
Ila ushujaa wangu ni kukutegemea wewe
Najua hakuna shujaa pasipo na maadui
Najua hakuna ushindi pasipo na mapambano
Siogopi mapambano, siogopi maneno
Siogopi masimango nataka kuwa shujaa
Najua dhahabu safi, husafishwa kwa moto
Najua ushindi wangu utakuja nitashindaa
[Verse 6]
Napenda kujifunza kwa tai niliyemfananisha na wewe
Tai hujenga nyumba yake juu ya maporomoko makali
Ambako nyoka na hatari haviwezi kufika huko
Tai hujali makinda yake yakiwa madogo
Tai ajengapo nyumba yake hujengea miti yenye miiba mikali
Juu yake hufunika manyoya lakini anajua nini anafanya
[Verse 7]
Ukifika wakati makinda yake yamekomaa
Taii huyanyima chakula yatoke ayafundishe kuruka
Yanapoendelea kukataa hupuliza manyoya
Miba alioweka huwalazimisha kutoka
Lengo la tai si kuyaumiza makinda yakee
Lengo la tai ni kuyafundisha kuruka juu
[Chorus]
Yakitoka nje (Aah) huyabeba mgongoni (Aah)
Hupanda nayo juu (Aah) kisha huyaachia (Aah)
Yanahangaika (Aah) kutafuta mama yao (Aah)
Nguvu zao zikiisha (Aah) mama yao hutokeza mbele (Aah)
Kwa zoezi hilo (Aah) hujifunza kuruka (Aah)
Ndipo hugundua (Aaah) nia njema ya mama yao (Aah)
Nawe Bwana wangu (Aah) nibebe kama tai (Aah)
Nguvu zangu zikiisha (Aah) nibebe kama tai (Aah)
Nawe Bwana wangu nibebe kama tai
Nguvu zangu zikiisha nibebe kama tai
Nibebe, nibebe kama tai
Written by: Ambwene Mwasongwe