Featured In
Similar Songs
Lyrics
[Verse 1]
Alright
Tisini na nne, march fifteen
Beginning of my world
Nilipozaliwa nikadondoka chini
Hakukua na kitanda kwa ward
[Verse 2]
Basi mgongo wa mama nikaufanya godoro
Na kilichonikuza mihogo na viporo
Nilipelekwa shule ila bado nikawa mtoro
Kingereza nilichokalili labda tomorrow ama today
Zikafika time ya kubalehe
[Verse 3]
Nikayajua mapenzi
Nikagundua bila pesa siyawezi
Ni ujinga
Nikadondokea umachinga
[Verse 4]
Hapakuchi panakucha siku zikasogea pruuh
Mpaka Dar Es Salaama nikaanza jitegemea
Nyumbani baba na mama wakiniombea
Mwanetu nenda salama na ukipata rejea
Mmh na ukipata
[Verse 5]
Hapo akili ndo ikaanza kukomaa
Na nikajuta kwanini sikusomaa
Jinsi jua la utosi linavyochoma
Na usiku baridi ikanipa homa
Nusu inuchukue uhai mmh
[Verse 6]
Mi nimepitia mengi ndo mana sio mshamba wa helaa
Kwa ajili ya vitu vidogo sigombani na maselaa
We kubali kudharauliwa
Kukataliwa
Kupata majaliwa
[Chorus]
Kula kinacholiwa (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Basi kamata chupa fungua na mimina (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Lewa tukuone unavyocheza kichina (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Anayekupenda zaidi ni wewe (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Ata anayekujua zaidi ni wewe (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
[Verse 7]
Masikini na wanawe, tajiri na mali zake
Asie na shida nawe mwache aende zake
Usibweteke na ulicho nacho
Pia usiteseke kwa walicho nacho
Riziki mafungu saba pengine leo zamu ya sita
Kaza moyo epusha roho yakusita
[Verse 8]
We umezaliwa peke yako
Utakufa peke yako
Na utazikwa peke yako
So usiwaeleze shida zako
Ukidhani ndugu zako, kumbe ndo wabaya wako
[Chorus]
Wee komaa (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Basi kamata chupa fungua na mimina (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Lewa tukuone unavyocheza kichina (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Anayekupenda zaidi ni wewe (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Ata anayekujua zaidi ni wewe (Mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe