Lyrics

Siijui hii SMS, baby
Unahaki sikulaumu na unakila sababu
Kuni-command kuniuliza, "Huyu ni nani?"
Siku-command mume wangu ila nalinda pendo langu
Upo ndani ya imaya yangu ndo' maana nina hofu na zao langu
Uko sahihi ila inabidi uchunguze kwanza
Ukipata jibu ndo u-panic sio, "Pu" tu unavimba
Hayo si maneno mume wangu kuyanena mbele yangu
Unazipelekea hisia zangu kuhisi naibiwa zao langu
Mm, basi baby nakupa message usome
Na ukishasoma usilalamike
Usini-set mume wangu nataka kuipooza roho yangu
Suluhisho la moyo wangu mpigie upooze mtima wangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie mweke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie mweke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi
Chozi langu thamani lanitoka chumbani, eh
Namlilia nani kama si' wewe
Najua ni hasira zikipoa mpendwa utaelewa
Hata maji ya moto hupoa mapema yakipepewa
Usipoteze lengo mume wangu
Unataka kuzifumba mboni zangu
Mpigie huyo mwenzangu
Ili nijue kuwa siko peke yangu
Haya kachukue charger yangu
Ipo kule kwenye mkoba wangu
Ukisharudi tena kwangu
Uwe utafurahi mke wangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie mweke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi
Wooh! Ona sasa zimefutika namba
Zimefutika sms kwenye inbox
Aah, bwana baba umezifuta makusudi
Mbona mi mwanzo niliziona kwa macho yangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie (mm) mweke loudspeaker tumsikie (mm)
Haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi
Haiwezekani tupigie (sina namba)
Mweke loudspeaker tumsikie (si unajua zimefutika)
Haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi
Achana nayo
Mm! Sawa bwana
Written by: Elias Barnabas
instagramSharePathic_arrow_out