Top Songs By Ambwene Mwasongwe
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Lead Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Ambwene Mwasongwe
Producer
Lyrics
[Chorus]
Na, na namjua Mungu (Namjua Bwana)
Na na namjua
(Nam, nam, nam) Na, na namjua Mungu
(Namjua yeye) Na na namjua
[Verse 1]
Alionekana sura yake kama malaika
Moyo mweupe uliotulia akiwaza memaa
Ukimtazama alivyopendeza anavutia
Tabasamu lake hata mbinguni walilikubali
[Verse 2]
Kama pilipili iliyotiwa kidondani na mkorofi
Ndivyo furaha yake ilivyoondolewa na neno dogo
Kama pilipili iliyotiwa kidondani na mkorofi
Ndivyo amani yake ilivyoyeyusha na jambo dogo
[Verse 3]
Nikaukumbuka uwongo wa shetani kumdanganya Eva
Ukifanya hivi utayajua mema na mabaya
Wakajisahau mema tayari waliyajua
Nia ya shetani litaka wajue mabaya
[Chorus]
Nguvu ya kujua mabaya kuna madhara mengi
Ni heri moyo wako ungejazwa na mambo mema
Alipojua amepata kansa kafa mapema
(Hakuishi) Alipojua mesalitiwa akazimia
Alipojua kafukuzwa kazi kachanganyikiwa
Angemjua Mungu ngepata neema ya kumsaidia
[Verse 4]
Moyo wa mtu ni kichaka umehifadhi mambo mengi
Uchungu, wivu na husuda na dhambi na mabaya mengi
Mungu alipoumba mtu alitaka ajue mema tu
Hakuthubutu kabisa ajue na mabaya
[Verse 5]
Nguvu ya kufa mtu imebebwa kwenye ubaya
Mkila tunda hili mtajua mema na mabaya
Mkila tunda hili mavumbini mtarudi
Lilikuwa ni tunda lenye kujua mema na mabaya
Mema walishakuwa nayo Mungu hakuwa na shida
Shetani alichokifanya kuhakikisha wajue ubaya
Hapo kikawa chanzo cha kifo kikawa chanzo cha magonjwa
Kikawa chanzo cha kilio kikawa cha maumivu ooh
Ayayayaya, eeh, ayaaa, aah, ayayayaya
[PreChorus]
Na, na namjua Mungu
Na, na namjua
(Yeye ni chanzo cha amani) Na, na namjua Mungu
(Yeye ni mwaminifu) Na, na namjua
Mungu wangu uuh
[Chorus]
Nguvu ya kujua mabaya kuna madhara mengi
Ni heri moyo wako ungejazwa na mambo mema
Alipojua amepata kansa kafa mapema
Alipojua mesalitiwa akazimia
Alipojua kafukuzwa kazi kachanganyikiwa
Angemjua Mungu ngepata neema ya kumsaidia
[Chorus]
Nguvu ya kujua mabaya kuna madhara mengi
Ni heri moyo wako ungejazwa na mambo mema
Alipojua amepata kansa kafa mapema
Alipojua mesalitiwa akazimia
Alipojua kafukuzwa kazi kachanganyikiwa
Angemjua Mungu ngepata neema ya kumsaidia
Written by: Ambwene Mwasongwe