Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Hawa
Vocals
Diamond Platnumz
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Diamond Platnumz
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Bob Junior
Producer
Lyrics
Vipi mizigo umeshaweka tayari mmh, aah
Sijechelewa nkajaachwa na gari mmh, aah
Basi jikaze usilie mpenzi aah
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi aah
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma sema ntafanya nini na pesa sina
Nakuonea na huruma bora niende mjini kusaka tumaa
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibajia waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea
Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasii
Ukumbuke na moyo, utajawa na simanzi
Ntakapokuwa nakwenda shambani, afu niko peke yangu honey
Ntapokuja kuwa na majirani nitaumia
Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani
Sina wakunitua nyumbani nitalia
Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo
Hata mwenzako sijawahi kufika Dar huu ndio mwanzo
Pili nakwenda na sijui pa kukaa wala mavazi
We niombee niepushwe na balaa na maradhi
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea
Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi
Usisahau kama mkeo na wana umetuacha na dhiki
Ila usijali ila naomba chunga sana ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki
Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo nyumbani na wana umetuacha na dhiki
Ila usijali ila naomba chunga sana ogopa na ma
Ukifika salama tukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo nyumbani na wana umetuacha na dhiki
Ila usijali ila naomba chunga sana ogopa na ma
Written by: Diamond Platnumz