Top Songs By Kontawa
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Kontawa
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Abdu Hamid
Composer
Lyrics
[Verse 1]
Kabla sijaswitch life
Hukupindua meza
Kipindi nauza mtumba
Natembea na nguo kariakoo magereza
[Verse 2]
Yaani kipindi sina good life
Hukuwahi kunibeza
Eeh ulinambia nitafute sana pesa
Kama vile mimi ndo nimepoteza
[Verse 3]
Chumba kimoja cha kupanga
Kuna doti moja tu ya kanga
Kuna kipindi nilisanda
Mpaka nikatamani nikupeleke kudanga
[Verse 4]
Baby maisha tuliyoishi
Tusingetoboa bila ubishi
Nlivyohustle sikufichi
Hadi nikinunua ugomvi nilikuwa nadai risiti
[PreChorus]
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Kwao tumetoboa
Amini kwamba tumetoboa
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Kwao tumetoboa
Amini kwamba tumetoboa
[Chorus]
Sikuachi mpaka milele
Mungu ametuona leo tuna mapeni
Piga kazi wee songa mbele
Mungu Ametuona leo zamu ya mi na wee
[Verse 5]
Najua haya maisha bila mwiko huwezi ukasonga mbele
Hata kama hupendi watu lazima utafute mchele
Waliotusema vibaya wanatuonea gere
[Verse 6]
Sisi tunafuga ng'ombe wao wanafuga nywele
Baby kipindi sina pesa uliposikia njaa
Uliziba masikio, eh
Leo nimepata pesa, nianze kukukataa staki laana kama hiyo, eh
[Verse 7]
Ukitaja watu wasiocheat me na we tumebakia
Haupendi pombe lakini una mguu wa bia
Embu sema unachotaka mi ntakufanyia
Hata usipoona siku zako mi ntakutafutia
[PreChorus]
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Kwao tumetoboa
Amini kwamba tumetoboa
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Kwao tumetoboa
Amini kwamba tumetoboa
[Chorus]
Sikuachi mpaka milele
Mungu ametuona leo tuna mapeni
Piga kazi wee songa mbele
Mungu Ametuona leo zamu ya mi na wee
Written by: Abdu Hamid