Music Video

Kontawa : Dunga Mawe ( official Music Video)
Watch Kontawa : Dunga Mawe ( official Music Video) on YouTube

Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Kontawa
Kontawa
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Abdu Hamid
Abdu Hamid
Composer

Lyrics

[Verse 1]
Anaitwa dunga mawe
Mwanangu wa utoto
Katika kitu nakumbuka
Alipitia changamoto
[Verse 2]
Mwanangu dunga mawe
Alikuwaga kibokoo
Na sura yake ilitumika
Kutishia watoto, eeh
[Verse 3]
Oya huyo mwanangu alikuwa msela
Alishawahi kufungwa akatoroka jela
Maisha yake visanga yani mpelampela
Asa ngoja niwape movie hilo lilikuwa trailer
[Verse 4]
Kuna kipindi dunga mawe si alipata mwali
Tukaenda hadi ukweni si kutoa mahali
Baada ya vitu kukamilika tulivyopewa mwali
Akamvizia baba mkwe akamwibia mahari
[PreChorus]
Alianza kuvata bangi na miaka saba
Ulivyofika wa nane akaanza kukaba
Sababu ya hali ngumu kakosa msaada
Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa
Ndugu wa karibu hawakumpa faraja
Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa
[Chorus]
Aah aah (Anaitwa dunga mawe)
Aah aah (Mwanangu dunga mawe)
Aah aah (Anaitwa dunga maawe)
Aah aah (Mwanangu dunga mawe)
[Verse 5]
Ukimletea unyonge lazima aruke nawe
Bora ukabwe na tonge ila sio dunga mawe
Utafanya kitu gani hili umfanye apagawe
Kashaoga matusi mpaka akaamua anawe
[Verse 6]
Ile siku dunga mawe akiamka vizuri
Tena ukamkuta kwenye mood
Anaweza agiza bia mbili, afu akakupa mia mbili
Kisha akasema kwamba chenji inarudii
[Verse 7]
Demu wake dunga mawe alikuwa na mimba
Yapata kama miez tisa
Kwa kuwa pesa ya uzazi ilimshinda
Ikabidi awe anapiganisha
[Verse 8]
Akamwambia kwamba mpenzi wake kuwa amepata safari
Anaenda kupambana hili mambo yawe shwari
Na atakaporudi watakwenda hospitali
Aahh
[Verse 9]
Kumbe alipanga kwenda kuiba huko sehemu za mbali
Ndipo akakamatwa na watu wenye asira kali
Wakamshushia kipigo, kipigo juu ya kipigo
Namwisho wakamchoma na mipira ya magari
[Chorus]
Aah aah (Anaitwa dunga mawe)
Aah aaah (Mwanangu dunga mawe)
Aah aah (Anaitwa dunga maawe)
Aah aah (Mwanangu dunga mawe)
[PreChorus]
Alianza kuvata bangi na miaka saba
Ulivyofika wa nane akaanza kukaba
Sababu ya hali ngumu kakosa msaada
Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa
Ndugu wa karibu hawakumpa faraja
Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa
[Chorus]
Aah aah (Anaitwa dunga mawe)
Aah aaah (Mwanangu dunga mawe)
Aah aah (Anaitwa dunga maawe)
Aah aah (Mwanangu dunga mawe)
Written by: Abdu Hamid
instagramSharePathic_arrow_out