Lyrics

[Chorus]
Natamani sana niwe kama Bwana mtu mwema sana aliyejikana
Niwe mpole niache ya kale nitazame mbele daima milele
Niwe mtiifu tena mwaminifu, mtakatifu asiyejifu
Mnyenyekevu na mvumilivu mtu mtulivu asiye na wivu
[Verse 1]
Bwana ulikuja duniani hapa
Kuleta ukombozi kwa kila kilichopotea
Ulianza na mimi niliyedhaifu
Ukaniinua kutoka matopeni
Wewe ulikuja kuleta suluhu
Ya makosa yote mwanadamu aliyokosea
Ulikuja kutibu kosa la mwanaume
Alilolifanya bustani ya Edeni
[Verse 2]
Mwanaume akikosea dunia yote huyumba
Mwanaume akikosea watu hujuta
Kila jambo ulionalo linayumba duniani
Limetokana na makosa ya mwanaume
[Bridge]
Leo natamani
Niweze kuwa kama wewe Bwana
Niweze kushinda yote magumu
[Chorus]
Natamani sana niwe kama Bwana mtu mwema sana aliyejikana
Niwe mpole niache ya kale nitazame mbele daima milele
Niwe mtiifu tena mwaminifu, mtakatifu asiyejifu
Mnyenyekevu na mvumilivu mtu mtulivu asiye na wivu
[Verse 3]
Nimevutiwa na historia yako
Wewe Bwana wangu Yesu ni wa ajabu
Kabla ulimwengu haujakuwako
Ulikuweko miaka mingi ya nyuma
Umeishi na wapole, umeishi na watakatifu
Umeishi na wanyenyekevu kama Henoko
Umeishi na watu wa kila aina
Wenye maombi na upako kama Musa
[Verse 4]
Pia umewahi kutana na wakaidi
Kama Farao na watu wenye roho ngumu
Una uzoefu wa kuishi na watu
Wenye tabia ngumu hiyo ndiyo sifa yako
Naamini Leo ukiwa ndani yangu Bwana
Nitaweza kushinda maisha yote
Kaa kwangu uniongoze mimi
Natamani sana kuwa kama wewe
[Bridge]
Niwezeshe wewe Bwana wanguu
Nataka kushinda yoote
[Chorus]
Natamani sana niwe kama Bwana mtu mwema sana aliyejikana
Niwe mpole niache ya kale nitazame mbele daima milele
Niwe mtiifu tena mwaminifu, mtakatifu asiyejifu
Mnyenyekevu na mvumilivu mtu mtulivu asiye na wivu
[Verse 5]
Nataka kufuata nyayo zako
Nataka kufuata hatua zako
Nataka kufuata upendo wako
Ulioacha enzi kuja kwetu hapa
Ulimpenda mwanadamu asiye na sifa
Ulimpenda mwanadamu asiye na vigezo
Ni upendo th uliokugharimu maisha
Umkomboe yeye kulipa deni lake
Written by: Ambwene Mwasongwe
instagramSharePathic_arrow_out