Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Goodluck Gozbert
Goodluck Gozbert
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Goodluck Gozbert
Goodluck Gozbert
Songwriter

Lyrics

Unaona kama kila unachogusa kimeharibika
Ujasiri wa kusema tena umetoweka
Maana kila unalosema wewe kama unakosea
Umechanganyikiwa ni Mungu ajua unayopitia
Na ukisema ueleze wengi kwao ni furaha
Wewe mwombe Mungu ubaki kimya
Na mengi umevumilia, moyo umenyong'onyea
Hapo ulipo sasa ng'ang'ania tena
Na Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda
Zipo nyakati za furaha nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe
Zipo nyakati za furaha nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe
Moyo wako una majeraha haufaii
Tena unasubiri kauli ya mwisho ya Mungu
Wapo wanaojua we huna mtoto
Kwa kejeli wanaulizaga ana umri gani
Tena wanaojua umefukuzwa kazii
Kwa kejeli wanaulizaga bosi wako yupo
Ila nakwambia hayatodumu ni nyakati tu
Hautobaki hapo haya ni mapito
Jipe moyo tazama juu, mwombe Mungu ujasiri
Ni mapito tu jipe moyo mkuu
Japo huna nguvu yakumwomba mwishie Mungu
Ni mapito tu jipe moyo mkuu
Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda
Zipo nyakati za furaha nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe
Zipo nyakati za furaha nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe
Wewe, wewe, wee, ooh
Hata wakizusha maneno ya uongo wakakwambia umemwasi Mungu (Ni sawa hawajui unakopita)
Wakaja na unabii wakasema umefika mwisho wako wee (Ni sawa hawajui unakopita)
Ooh wakainuka ndugu wa karibu wakakusema hovyo hovyo hovyo hovyo (Ni sawa hawajui unakopita)
Ikawa kila kitu ni kimya marafiki ni kimya (Ni sawa hawajui unakopita)
Kama ndoa ni yako lakini ndani ni uadui (Ni sawa hawajui unakopita)
(Ilaaa) Zipo nyakati za furaha, nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha, nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha, nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe
Written by: Goodluck Gozbert, Goodluck Gozbert Wiki
instagramSharePathic_arrow_out