Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Thimos Chelula
Thimos Chelula
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Tulikotoka ni mbali, tukitazama nyuma
Asingekuwa Bwana, tusingefika hapa
Yale tuliyoyapitia, hayakutuacha tulivyo
Haikuwa rahisi ni mkono wa Bwana
[Verse 2]
Pengine yalikuja kama mema mwisho ukawa mbaya
Pengine yalikuja kama mabaya kumbe yanakusudi
Lakini katika yote hayo tulikuona Bwana
Ukitetea maisha yetu dhidi ya hatari mbaya
[Verse 3]
Tulikutana na hatari mbaya, tukajua ni mwisho
Tulikutana na majanga mengi, tukajua hakutakucha
Lakini katika yote hayo, wewe ulisimama
Kutetea maisha yetu, yasidhulumiwe
Yah, yah, yah ayayaya, uuh
[Verse 4]
Kaa nasi Bwana, safari bado ndefu
Tunakumbuka mengi tuliyoyaona nyuma
Tunakumbuka mengi tuliyoyasikia
Tulipitia magumu yaliyotuchanganya sana
Tulipitia mengi yaliyotuvuruga mioyo
Tunakumbuka ndugu zetu tuliyowaacha nyuma huko
Tulitamani leo hii, tungekuwa nao
[Verse 5]
Namkumbuka huyu alivyolia (Eehh, eehh)
Alipowakumbuka ndugu zake (Eehh, eehh)
Alitukaribisha kwao, ayayaya
Akasema maneno haya
Jamani karibuni nyumbani hapa ndipo kwetu
Kwanzia huku hadi kule hizi ni nyumba zetu
Na kama mnavyoona wenyewe hawapo
Nyumba imebaki kimya na sisi tunaishi mbali
[Verse 6]
Jamani karibuni nyumbani hapa ndipo kwetu
Kwanzia huku hadi kule hizi ni nyumba zetu
Na kama mnavyoona wenyewe hawapo
Nyumba imebaki kimya na sisi tunaishi mbali
[Bridge]
Ayayayaya aya
Ayayayaya aya
[Verse 7]
Mwengine alisimama akatafakari
Akapiga hesabu za maisha yake
Akaona mambo yake hayako sawa
Akatazama nyuma alikotoka akasema
[Verse 8]
Jamani niombeeni mambo ni magumu
Hali ninayopitia hata sielewi
Mwenzangu kabadilika siyo kama zamani
Hali inayoendelea sijui itakwisha lini
Ayayayaya
[Verse 9]
Ni kweli tunapita, ni kweli yapo mengi yanayotusibu
Ila Mungu wetu yuko palepale
Ila wema wake Bwana uko palepale
Katika yaleyale wengine wanayolia sana
Wapo wengine bado wanaimarishwa
Katika yaleyale yanayowatoa roho wengine
Katika hayohayo wengine wanasonga mbele
Haa
[Verse 10]
Daudi anasema katika magumu yote
Nalimwona Bwana kasimama mbele yangu
Kumbe tatizo letu liko kwetu wenyewe
Tunaona magumu hatumuoni Bwana
[Verse 11]
Tatizo haliko kwa Mungu tatizo liko kwetu
Wala haliko kwa shetani tatizo liko kwetu
Tatizo ni sisi wenyewe vile tunavyoona
Hilo ndilo tatizo letu linalotusumbuaa
[Outro]
Songa mbele, usitazame nyuma
Mtazame Bwana
Atakutia nguvu atakuinua na wewe
Usitazame nyuma mpendwa mtazame Bwana
Written by: Ambwene Mwasongwe
instagramSharePathic_arrow_out