Lyrics

[Verse 1]
Hata nikiwa sina chakula
Isinifanye kusahau
Ulinilisha nikasaza
Hata nikiwa sina mavazi
Isinifanye nikufuru
Na kusahau umeniweka hai
[Verse 2]
Ona wapo marafiki
Wanakosa kula na kuvaa
Hawalalamiki wanakushukuru tu
Mimi eeh, nilikupa nini Baba
Cha kunipa kibali
Kwa siku zilizofurahisha
[Verse 3]
Tabu kidogo zisifanye nikusahau
Umeshatenda mengi nikiwa hapa
Eeh! Shida itapita bado kidogo
Ikiwa nitachoka ninue
[Chorus]
(Nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
(Aahh nipe) Kukumbuka wema
Nipe, wako
[Chorus]
(Nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
[Verse 4]
Hata kwenye bonde hili la mauti
Nakumbuka nilikuita
Na wewe ukaitika, Baba
Kutegemea akili zangu
Na mawazo yangu
Kutanifanya niendelee, ah niendelee kulalamika
[Verse 5]
Kuna kipindi najisahau
Na kujivunia mafanikio
Wengine naona takataka
Nikumbushe mi ni mtu tu
Na dunia tunapita
Uhai wangu si faida bila wewe
[Verse 6]
Mungu wewe nii mkuu
Kuliko vile nakutazama Baba
Unisamehe, unisamehe
Kuna nyakati nadhani, hii dunia labda ni ya ushindani
Natumia akili zangu za ndani, ila bado nashindwa kuendelea
Nikumbushe nisidhani, wakifanikiwa tuna upinzani
Nifundishe kuwaombea amani
Na utatenda kwa wakati
[PreChorus]
Na ikiwa kama nikisahau
Unikumbushe mi mtoto wako
Si ama nikisahau
Unikumbushe mi mtoto wako
[Chorus]
(Nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
Nipe, wako
[Chorus]
(Nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
(Ooh nipe) Kukumbuka wema
(Wowowo) wako
(Oh wewe wewe) Kukumbuka wema
(Ooh woo) Kukumbuka wema, wako
(Aah iye) Kukumbuka wema, wako
[Chorus]
(Hata nisipofanikwa) Kukumbuka wema
(Nikarudi kwenye dhiki) Kukumbuka wema
(Kupoteza marafiki) Kukumbuka wema
Unikumbushe kumbushe tu (Wako)
(Baba yangu) Kumbuka wema
(Ooh Nikumbuke pia) Kumbuka wema
(Ooh fadhili zako) Kumbuka wema, wako
(Unikumbushe Jehova) Kumbuka wema
(Unikumbushe Masihi) Kumbuka wema
(Kwamba uliniumba niwe) Kukumbuka wema, wako
Written by: Goodluck Gozbert, Goodluck Gozbert Wiki
instagramSharePathic_arrow_out