Lyrics

[Verse 1]
Ooh ye dunia sasa i mashakani
Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa
Kwa gharama kubwa imejengewa ngome za kifahari
Ooh ye dunia sasa ni mashakani
Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa
Kwa gharama makubwa imejengewa ngome za kifahari
[Verse 2]
Mabomu ya kujitoa muhanga ni jambo la hatari
Umwagaji damu isiyo hatia ni jambo la kutisha
Yaliyonenwa na nabii Danieli sasa yanatimia
[Verse 3]
Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana
Atulize ghadhabu yake isiipate dunia
Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana
Atulize ghadhabu yake isiipate dunia
[PreChorus]
Eeh, lelelelelelele
Mteule uwe maacho
Ni siku za mwisho nasema
[Chorus]
Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho
Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia
Tusimame imara tujifungeni mikanda
Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele
[Chorus]
Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka
Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni
Uwe macho, hizi ni siku za mwisho
Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia
[Chorus]
Tusimame imara tujifungeni mikanda
Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele
Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka
Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni
[Verse 4]
Kutangatanga kwako wewe, mbona kwa kuchelewesha
Nachelewa kusema nawe, utafuna ulichopanda
Shika sana ulicho nacho, Yesu yu karibu kuja
Mwenye sikio asikie, roho asema na kanisa
[PreChorus]
Eeh, lelelelele
Ah yayayayaya
[Chorus]
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Muongo endelea kutenda dhambi, dunia ikujuee
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Mumbea endelea kusema umbea, vunja nyumba za watu
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Mchawi endelea kuroga sana, mchana peupee
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
[Verse 5]
Wachungaji tuelezeni, mwatupeleka wapi jamani
Mbona Asikofu mwanamume, ameoa mume mwenzie
Andiko hili latoka wapi, tena kwenye Bibilia gani
Watoto wetu wa kiume, tuwafiche wapi jamani
[Verse 6]
Wamama nao bila aibu, wazini na vijana wadogo
Sasa tutapataje kupona, ukimwi utatumaliza
[PreChorus]
Eeh, lelelelele
Ah yayayayaya
[Chorus]
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Kahaba endelea kufanya ukahaba, mpaka kwenye internet
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Malaya endelea kufanya umalaya, utakwenda na ngoma
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Washerati endelea kufanya dhambi, Yesu yuaja
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Mlokole endelea kujitakaza, Yesu yuaja
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
Shoga endelea kufanya ushoga, mpaka kwenye mtandao
Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi
[PreChorus]
Eeh, lelelelele
Jamani nasema
[Chorus]
Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho
Kwani yale yaliyotabiriwa sasa, yanatimia
Tusimame imara, tujifungeni mikanda
Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele
Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka
Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni
Uwe macho
Written by: Rose Muhando
instagramSharePathic_arrow_out