Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Lava Lava
Lead Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Lava Lava
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Bōnga
Producer
Lizer Classic
Mixing Engineer
Lyrics
Mwenzako jicho chongo, kwa mwengine sioni tena
Umenipa magongo nitembee, niache kuchechema
Tujiepushe na waongo, hawakosagi cha kusema
Ulinzi nguzo chuma dongo, penzi tuezeke na mahema
Penzi langu la kizigua nakupa taratibu
Na miuno nainengua washikwe na aibu
Nadhani hawajajua wewe ndo unaniharibu
Na mwaka huu mbona wataugua wakose wa kuwatibu
Wewe nipe mambo ya Pwani (Eti mwenzako nina nenge)
Kanga moja begani (Uno ulifunge tenge)
Mguu bara mguu Pwani (Kama unaruka senyenge)
Wanibinyie kwa ndani (Nitoke malenge-lenge)
Saula! (Mambo yaweke hadharani)
Saula! (Kwani unamuogopa nani)
Saula! (Uyaweke hadharani)
Saula! Yee (Kwani unamuogopa nani) Saula!
Kama karata umelamba dume, wengine garasa bado (Saula!)
Tikitaka kinyume nyume, mashuti kama Ronaldo (Saula!!!)
Kaliona Jiti kasaula kajitupa kwa kiwanja, kibichibichi kwa Kajala Masanja
Kweli npe nisivyopewa hadi nihisi raha ya dunia, nijione mwenye ngekewa mafisi waje ninunia
Nipost usiogope sa' unifiche Mobeto (Ahee), tena mashost na waropokwe tujichimbie magheto (Ahee)
Wee nipe mambo ya pwani, eti mwenzako nna nenge
Kanga moja begani, uno ulifunge tenge
Siku ya kufa nyani kinyozi kakosa wembe
Kule Mtwara nyumbani tunaitaga singege
Saula! (Mambo yaweke hadharani)
Saula! (Kwani unamuogopa nani)
Saula! (Uyaweke hadharani)
Saula! (Kwani unamuogopa nani) Saula!
Aah! kibinda (Aah kibinda nkoe), yeeh! ( Kibinda nkoe)
Fanya kujipinda-pinda (Aah kibinda nkoe), eh yeeh! (Aah kibinda nkoe)
Cheza ukiringa ringa (Aah kibinda nkoe), eeh! (Kibinda nkoe)
Zungusha nyonga madoido (Aah kibinda nkoe), kakupa mama (Kibinda nkoe)
Uno la Kofi Lomido (Aah kibinda nkoe), binua bandama (Kibinda nkoe)
Written by: Lava Lava