Lyrics

Nilie nae hana (Kasoro), ya nini nipashe (Viporo)
Uliniacha (Totoro) bila ya (Godoro)
Mpenzi kiberiti (Washa), siwezi kusaliti (Washa)
Yeye sabuni mie jiki (Washa), mie jiki (Washa), mie jiki (Washa)
Maji mwenzake kopo oh, tucheze kidalipo oh
Huko ulipo oh, salamu zikufikie
Yameandikwa maandiko usiibe mboga usilambe mwiko oh
Kurudi kwako ni ndoto ah, sitaki yajirudie
Nile naye kwa siku mara tatu kama mgonjwa wa homa
Nikiumwa na pona, dozi nzuri yaani ile kuona
Penzi ukalivika ngozi ya chatu, vya kupika ulichoma
Penzi ukaliunguza, unataka kurudi hapana, maana
Nilie nae hana (Kasoro), ya nini nipashe (Viporo)
Uliniacha (Totoro) bila ya (Godoro)
Mpenzi kiberiti (Washa), siwezi kusaliti (Washa)
Yeye sabuni mie jiki (Washa), mie jiki (Washa), mie jiki (Washa)
Mpenzi kiberiti (Washa), siwezi kusaliti (Washa)
Yeye sabuni mie jiki (Washa), mie jiki (Washa), mie jiki (Washa)
Ukiachwa achika, ukimwagwa mwagika
Ukitemwa temeka, penzi bovu yanini kung'ang'ania
Roho unaisononesha, moyo unaukondesha aah
Wakati hujapendeka, wako wengi wanaokutamani
Kaaga kaenda kwa mama (Mdogo), waja kumfumaga bar (Majogoo)
Ya nini kujisononesha, mtoto mdogo wajipaga pressure bure
Nile naye kwa siku mara tatu, kama mgonjwa wa homaa
Nikiumwa na pona, dozi nzuri yaani ile kuona
Penzi ukalivika ngozi ya chatu, vya kupika ulichoma
Penzi ukaliunguza, unataka kurudi hapana, maana
Nilie nae hana (Kasoro), ya nini nipashe (Viporo)
Uliniacha (Totoro) bila ya (Godoro)
Mpenzi kiberiti (Washa), siwezi kusaliti (Washa)
Yeye sabuni mie jiki (Washa), mie jiki (Washa), mie jiki (Washa)
Mpenzi kiberiti (Washa), siwezi kusaliti (Washa)
Yeye sabuni mie jiki (Washa), mie jiki (Washa), mie jiki (Washa)
Written by: Elias Barnabas
instagramSharePathic_arrow_out