Lyrics

Oh-wah, ah, oh-wah, oh-wah, ah, oh-wah
Oh-woah-woah-oh
Alisema mapenzi vita, mi na yeye tuungane kuwateketeza maadui, eti, maadui
Badala ya miezi kupita, aah, vikombe lazima vigongane, Na sio kwamba hayajui, eh, hayajui
Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo, ama kumtafuta mchawi ni nani ni kuongeza tatizo
Tuliapa tutakuwa wa ndani hadi paradiso, na tukatangaza kweupe mambo hadharani
Na tattoo ndo hizo, oh-oh-oh-oh-oh
Sitaki kuamini kwamba, lile kapu la mabaya yangu, halina hata machache mema, oh, mema
Nitakuwa mshamba, nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu, ili nionekane mwema
Japo mapenzi yanaumiza, I wish tusisemane (Vibaya), oh-le-le-le (Vibaya)
Ili kesho tusizikane (Vibaya) oh-no-no (Vibaya), usiwasikilize wapambe (Vibaya)
Wanachotaka maneno (Vibaya) ili kesho watuchambe (Vibaya), oh-oh-oh-oh (Vibaya)
Oh-wah, ah, oh-wah, oh-wah, ah, oh-wah
Oh-woah-woah-oh, mm-mm
Nitunzie siri zangu, nami nitunze zako za miaka rudi nenda, kuna leo na kesho, mm-mm-mm
Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako hawawezi kukupenda, wanakuvuta uwe kichekesho, mm-mm
Maana hata ukisambaza, picha zangu za aibu ni sawa, hata hunikomoi
Na hata utupu wako ukiutandaza kwa watu wangu wa karibu sio dawa, hujengi hubomoi, eh-eh-eh-eh
Mama kuna kamchezo, mtunze mtoto wako, na watu wenye majungu, majungu
Nilikubali kuviacha vya dezo, sababu ya mapenzi yako, nikaachana na mzungu, mzungu
Maneno yao utadhani wanakutetea, kumbe tudhalilishane wanachongojea
Usiwape faida wambea, na ni kama kawaida nakuombea
Sitaki kuamini kwamba, lile kapu la mabaya yangu, halina hata machache mema, oh, mema
Nitakuwa mshamba, nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu, ili nionekane mwema
Japo mapenzi yanaumiza, I wish tusisemane (Vibaya), oh-le-le-le (Vibaya)
Ili kesho tusizikane (Vibaya) oh-no-no (Vibaya), usiwasikilize wapambe (Vibaya)
Wanachotaka maneno (Vibaya) ili kesho watuchambe (Vibaya), oh-oh-oh-oh (Vibaya)
Oh-wah, ah, oh-wah, oh-wah, ah, oh-wah
Oh-woah-woah-oh, oh-oh-oh-oh
Written by: Harmonize
instagramSharePathic_arrow_out