Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Lead Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Mmh, Haleluya
Huuapia moyo ntakulinda
Maana najua kwamba kuna chemichemi
Ntakujengea boma uwe salama
Adui akija asikuweze
[Verse 2]
Usiruhusu maneno yakuvuruge
Usiruhusu hasira ikae kwako
Ntamuweka mlinzi awe ngome yako
Akupiganie ubaki salama
[Verse 3]
Bwana naomba utete nao wale wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sistaili kubishana nao
Sitaki kupambana nao
Nisije nikakosea wakanilaumu
[Verse 4]
Maana wameshavuta upinde wapo kwenye mangojeo yao
Wamenuna wamekunja sura wanahasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru ni kwamba hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee waninase
[Verse 5]
Usiache mguu usogezwe unase kwenye mitego yao
Weka mgojenzi, kinywani mwangu anilinde nisiropoke
[Chorus]
Hili ni ombi langu kwako Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe hata uwapo gizani akulinde
Wewe ni wimbo wangu tena dawa ya moyoni mwangu
U fahari yangu nikupate vyote nimevipata Mungu
Haa, haa, haa, haa, haa, haa
[Verse 6]
Nifanye kama Yusufu uliemuona muota ndoto ukam-bariki
Wewe ulimuona waziri mkuu tofauti na wanadamu
Wakamtazama vingine walivyoweza
Baba yake alimuona mpelelezi awapeleleze ndugu zake
Ndugu zake walimwona ni mmbea wakamtupa shimoni
[Verse 7]
Wamediani wakamwona biashara wakamuuza kwa Potifa
Mkewe Potifa kamtamani akamuona kijana mzuri
Wafungwa wenzake wakamsahau wakifikiri ni mhalifu
Wewe uliona ndoto ndani yake ukamfanya waziri mkuu
Nami nifanye kama Yusufu
[Chorus]
Hili ni ombi langu kwako Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe hata uwapo gizani akulinde
Wewe ni wimbo wangu tena dawa ya moyoni mwangu
U fahari yangu nikupate vyote nimevipata Mungu
Haa, haa, haa, haa
Haa, haa, haa, haa
[Outro]
Haa, haa, haa, haa
Haa, haa, haa, haa
Haa, haa, haa, haa
Haa, haa, haa, haa
Haa, haa, haa, haa
Kwako nitaburudika
Written by: Ambwene Mwasongwe
instagramSharePathic_arrow_out