Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
BRIGHT
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Rashid Said Madegadega
Composer
Lyrics
[Verse 1]
Ahsante Mungu wangu kwa siku ya leo
Umenivusha pakubwa kuiona leo
Kuna watu tulikuwa nao, lakini sasa hatupo nao
Kazini kwangu umenipandisha cheo
Wafanyakazi wenzangu hawataki niwe na cheo
[Verse 2]
Marafiki wamenitenga, wanafki wamenitega
Nikosee wanicheke
Nashukuru upo upande wangu uuh
Unanipaga na ridhiki yangu uuh
Silalamiki nikikosa, naamini nitapata, ipo siku yangu tu
[PreChorus]
Naandamwa na maadui kila upande
Sio rafiki hata ndugu hawataki nipande
Wakikusaidia mpaka wakutangaze
Baba nioneshe njia nataka niwashangaze yeeh
[Chorus]
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
[Verse 3]
Naishi Mungu anavyotaka siishi kwa ndoto yangu
Vita ni kali mishale yote imenyooshwa kwangu
Shida njaa, madeni yote yangu
Nilitegemea cha ndugu, sasa imekula kwangu
[Verse 4]
Kodi imekata nadaiwa pesa ya pango
Sina kila kitu sina hata nyendo
Waya mkali jua linagonga kila engo
Nimkope nani labda nitaziba pengo
[Verse 5]
Maneno ya watu mali zipo kwa waganga
Nimwage damu, nizike mtu kwenye mchanga
Nichinje mbuzi nami nijaribu kuwanga
Labda nitatoboa aah
[Verse 6]
Yule rafiki sasa amegeuka adui
Ulompandisha eti sasa hakujui
Penye ridhiki hapakosi chuki
Unaemuamini ndio atakuchoma mkuki
[Verse 7]
Nashukuru uko upande wangu uuh
Unanipaga na ridhiki yangu uuh
Silalamiki nikikosa, naamini nitapata
Ipo siku yangu tu
[PreChorus]
Naandamwa na maadui kila upande
Sio rafiki hata ndugu hawataki nipande
Wakikusaidia mpaka wakutangaze
Baba nioneshe njia nataka niwashangaze yee
[Chorus]
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Bila Mungu sitoboi, ooh ooh
Written by: Rashid Said Madegadega