Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ay Masta
Ay Masta
Performer
A.Y.
A.Y.
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Allen Yessayah
Ambwene Allen Yessayah
Composer

Lyrics

Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)

Wengi wao wanatabasamu, wanaongea kwa nidhamu, wanajifanya watu wa karibu kumbe hao ndo sumu
Wanajifanya wana upendo ilmarid wawe kando, wameweka mbele dini fungo moyo usiwaamini
Si unakumbuka alikufaa kwa dhiki? (Kweli) Enzi zile upo nae marafiki
Aha, yuko wapi sasa hayupo tena ashasaliti kweli akufaae kwa dhiki mara nyingine ni msaliti
Alishatembea na mkeo kwa gia ya urafiki, shoga yako kwako habanduki mmeo akakutaliki
Unajuta ye anacheka kwani ndoa keshaivuruga, mmeo ametimua ye keshatawala nyumba
Baba na nyumba ndogo watoto wanalia mateso, anadiriki hata kuwakana hana huruma hata kidogo
Haina mshangao watu wa aina hii wapo, sio sehem zingine hata hapa ulipo wapo
Jirani yako mchana mnacheka usiku mwanga, nia yake kuona life oh inapinda
Dili zote zigime mipango igonge mwamba afya yako bandika bandua ya magonjwa itatamba
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Dunia inavunda vvu walimwengu hawashikiki (Wengi wanapenda ngono lakini kuzaa hawataki)
Wengi nacheka nao tu lakini sio kwa dhati, hivyo ni kama nipo gizani halafu nalamba ncha ya mkuki
Wengi wanatoa mimba wengine wanatupa watoto, ungekuwa wapi mama yako angekutupa enzi hizo
Imani hakuna ndani ya maovu yasio na mwisho, nakata tamaa akili inachoka moyo mzito
Machoni kama watu kumbe wamejaa unyama tu, kaa chonjo chunga sana napo akili kichwani tu
Hapendi kukuona unatesa juu yako mzigo chuki, ameshatega mabaya mitego ndo haikamatiki
Hapendi kuona unawini hapendi kuona unafuraha, raha yake kuona umezungukwa na karaha
Hana raha anapoona mambo safi kiuchumi, moyo utakuwa shwari tu pale una hali duni
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Huyo ndo mwanadamu anapowini tu dharau, napo ni mgumu kuelewa mwepesi kusahau
Wanajionyesha ana huruma, mpole na mkarimu, na aliye mstari wa mbele kutoa ahadi tamu
Usimpa nafasi hata ajue zako habari, hana jema chunga sana hana ujio wa heri
Hataki kabisa kuona unavuta hewa hii lakini, wapi mipango inabaki zii
Ni rahisi kwake kupata mali kwa njia ya kuua, haya mambo hi hali nadhamni wote mnaijua
Mlale pema mliouwawa mkidai zenu haki, sisi bado tupo duniani hatujui lini tamati
Jasho la mnyonge huwa ni neema kwa wachache, ni kilio cha fukara chenye lengo haki nipate
Stuka huko tunakokwenda kunatisha, kwani itakuwa ndoto watu kutenda mema kabisa
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Machoni kama watu, mioyoni hawana utu (Imani imetoweka, mabaya yanaongezeka)
Written by: Ambwene Allen Yessayah
instagramSharePathic_arrow_out