Top Songs By Rayvanny
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Rayvanny
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Rayvanny
Songwriter
Raymond Shaban Mwakyusa
Composer
PRODUCTION & ENGINEERING
Lizer Classic
Producer
Lyrics
Sifa kwa Mola wangu Maulana, kwa mengi aliofanya, hadi mi na we kukutana, kisura
Sijapanga kudanganya, nasema ukweli mama, kisa nakupenda sana, kisura
Umesema wanipenda, ila maisha yangu maseke
Michicha milenda, ndo menu yangu na ya kuku mateke
Yaani chenga, kila siku kilio saa lini nicheke
Sina tenda, ugali buguruni mboga temeke
Nafurahi umeniridhia, niwe na wewe kimwali
Maisha yangu mitihani, isoisha maswali
Ukifika nyumbani vumilia, maana hali sio shwari
Asubuhi mchana pakavu, jioni ndo kula futali
(Tena huku kwetu) Muda wowote mateja wanatinga
(Viwaro vyetu) Ukifua kumbuka kuvilinda
(Huku kwetu) Muda wowote mateja wanatinga
(Mwali wee) Suala la nyumba na gari mimi
Bado, (Mi bado), mi bado, (Ndo kwanza nimepanga) Bado, (Iyee), mi bado
(Sina hata kiwanja) Bado, (Iyee), mi bado
(Kulipa kodi majanga) Bado, (Mimi bado), mi bado
Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro
Ghetto na mkeka tu hakuna kitanda shuka wala godoro
Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya Comoro
Ila nimeshakupa, nimeshakupa mtima-mtima
Ukija kususa, utanizika mzima-mzima
Nimeshakupa eh, nimeshakupa mtima-mtima
Ukija kususa, utanizika mzima-mzima
(Tena huku kwetu) Muda wowote mateja wanatinga
(Viwalo vyetu) Ukifua kumbuka kuvilinda
(Huku kwetu) Muda wowote mateja wanatinga
(Mwali wee) Suala la nyumba na gari mi
Bado, (Mi bado), mi bado, (Ndo kwanza nimepanga) Bado, (Iyee), mi bado
(Sina hata kiwanja) Bado, (Iyee), mi bado
(Kulipa kodi majanga) Bado, (Mimi bado), mi bado
Suala la nyumba na gari mi bado, (Mi bado), mi bado
(Ndo kwanza nimepanga) Bado, (Iyee), mi bado
(Sina hata kiwanja) Bado, (Iyee), mi bado
(Kulipa kodi majanga) Bado, (Mimi bado), mi bado
Written by: Raymond Shaban Mwakyusa