Top Songs By Queen Darleen
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Lava Lava
Vocals
Queen Darleen
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Queen Darleen
Transcription
PRODUCTION & ENGINEERING
RashDon
Producer
Lyrics
[Verse 1]
Eti Lava utaoa lini, mbona unazingua?
Wazuri wengi mjini, wezi wanachukua
We kutwa ubishoo
Nywele kuchange mitindo, wanakuona wafoo
Kila siku uko single
Moyo wa kupenda sina, ya nini nijipe homa
Si huyu ni mwana Stamina, rafiki yake Roma
Si unajua ndoa majaliwa, nasubiria apange Maulana
Atanitunukia, bado naula ujana
[Verse 2]
Ujana maji ya moto utakuunguza (Nitakuunguza)
We pita peku mpoto tutakuunguza
Kwanza kuolewa (Raha), oh nah, nah wili-wili
Ona mume wangu hii (Spa), atumiliki wawili-wili
Umenikumbusha kule Insta udaku
Wanasema mume umekwara ati umefuata hela
Ukakubali kuolewa mitara
[PreChorus]
Hutanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini? Bora niwe bachela
[Chorus]
Sitaki kujifunga, kujibana-bana (Niwe bachela)
Kwanza naona mapenzi faida hayana (Bora niwe bachela)
Huo ni utoto unajidanganya (Niwe bachela)
Unayoyafanya mwisho hayana (Bora niwe bachela)
[Verse 3]
Dala Darleen acha kunichachafya, uliza kilomkuta Dangote
Sijui kagombana na Tanasha ametu-unfollow wote
Mapenzi ya siku hizi shemeji Lokole mwongoza umbea
Mkigombana tu kashatizi Insta nzima yameshaenea
Ndio maana nimetulia navuta pumzi staki kuenda mbio
Mambo ya kujifanya hodari eti mjuzi (Ujuzi huo kwio)
Tukiachana na yote, mimi bado sikuungi mkono
Wasafi wote mnaonekana mnapenda ngono
[PreChorus]
Hutanishauri mimi (Wakati wangu ndo sasa)
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini (Acha nile bata)
Nijipe stress za nini? Bora niwe bachela
[Chorus]
Sitaki kujifunga, kujibana-bana (Niwe bachela)
Kwanza naona mapenzi faida hayana (Bora niwe bachela)
Huo ni utoto unajidanganya (Niwe bachela)
Unayoyafanya mwisho hayana
[Outro]
Mabachela piga kelele (Wee)
Piga kelele moja (Wee)
Kelele mbili (Wee, wee)
Piga kelele tatu (Wee, wee, wee)
Wenye wapenzi piga kelele (Wee)
Walio oa (Wee)
Tulio olewa je? (Wee, wee)
Written by: Queen Darleen