Lyrics

[Verse 1]
Yale maneno uyasemayo, ona ndege wa angani
Wanakula, hawapandi na tena hawavuni
Ni sawa sikuelewa walinikiza vya nini
Walikula, imebaki, wengine wamekosa
[Verse 2]
Kumbe ipo maana, ya kushukuru kwa kidogo
Moyo wangu unalaumu ila shida waijua
Wapo wal'okosa kabisa
Na wanashukuru Mungu
Wewe kutaka ma fashion unamlaumu Mungu
Unanifanya moyo nitamani kua kama yule
Hali yangu duni nitadhalilika
[Chorus]
Mmh, mmh (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba (Aah moyo wangu)
Aah tulia-tulia usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba (Aah moyo wangu)
Aah tulia-tulia usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba
[Verse 3]
Wapo wengi, wenye shida
Huwajui, huwajui
Wako wengi, wenye dhiki
Huwajui, huwajui
Unajua dunia ni njia
Unataka kujenga ghorofa la kazi gani
[Verse 4]
Ata usipo salimia
Jua utazikwa chini, jeuri ya nini
Unanifanya moyo nitamani kua kama yule
Hali yangu duni, nitadhalilika
Nimeshafanya mengi kubatili faida haipo
Bora nimpe sifa Mungu
[Chorus]
Baki na amani moyo (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba (Aah moyo wangu)
Aah tulia-tulia usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba (Aah moyo wangu)
Aah tulia-tulia usikufuru Mungu (Aah moyo wangu)
Tulia-tulia, mengine ni ushamba
Written by: Goodluck Gozbert, Goodluck Gozbert Wiki
instagramSharePathic_arrow_out