Lyrics

Nisumbue-sumbue usikubali haraka-haraka mimi aah, mi staki kukuacha love naomba ujiamini iih
Hakuna mwingine mi najali maishanii aah (Nisumbue-sumbue usinikubali haraka)
Ila we pekee sitaweza kukuacha honey (Nisumbue-sumbue usikubali haraka-haraka)
Naomba uniweke ndani ya chupa kwako nifike kabisa mchumba nichizike, nife, nizikwe na wewe kabisa
Binadamu, me, nafahamu sijakamilika niponde kama wadau wa ze utamu kila dakika
Nitafurahi kama utanimwaga, nikija kwa gia za mkwanja, nitarudi kujipanga kiunderground kama Alphanga
Kukupa moyo ukinifanya niwe na wivu, kwa mfano nikituma meseji naomba uchelewe kunijibu
(Na sio lazimaa) Kila sehemu ninayokualika utokee, au kila simu ninayokupigia ewe malkia uipokee
Nyingine unaweza zichunia hiyo inaweza saidia kuniweka roho juu na kunijaza uchungu pia
Tusikutane leo mtaani halafu kesho eti uibuke ghetto, nizungushe ili nijitoe mwisho wa siku niingie mpeku
Usinikubali haraka sababu utaharibu mapenzi nami sitaki kukuacha au tuishie one night stand
Sijakupenda leo tu kwa sababu tumekutana nilikupenda long time hadi leo nakupenda sana
Nikikutazama napata hisia za kuoana sio kukudanganya kisha nikaishia kukuoa
Nisumbue-sumbue usikubali haraka-haraka mimi aah, mi staki kukuacha love naomba ujiamini iih
Hakuna mwingine mi najali maishanii aah (Unisumbue-sumbue usikubali haraka)
Ila we pekee sitaweza kukuacha honey (Unisumbue-sumbue usikubali haraka)
Usiniambie rangi uipendayo acha mwenyewe niitafute (Usitunzee), kila zawadi ninayokupa nyingine zitupe ili nijifunze
Ninapoingia ndani ya duka bei isishuke (Usijichubue) kwa kuwa wanazusha eti napenda ngozi nyeupe
Niimbie usiulize ya rado tu, mkere Fid Q ukiona hainiumizi bado ujue kwako nimefika full nimechizika boo
Sio kama ninapita tu, sijajipachika kama sticker nimekita kama tatoo
(Kama unanipenda nipendee iih) lakini usinikubali haraka, we ni jangwa mie ni mtende nimekuja kama sadaka
Wote walionikubali haraka hatukudumu tuliachana sitaki kuamini nina zali eti kwakuwa ninajulikana
Sijakupenda leo tu sababu tumekutana, nilikupenda long time hadi hii leo nakupenda sana
Nikikutazama napata hisia za kuoa na sio kukudanganya kisha nikaishia kukuoa
Nisumbue-sumbue usikubali haraka-haraka mimi aah
Mi staki kukuacha love naomba ujiamini iih
Hakuna mwingine mi najali maishanii aah (Nisumbue-sumbue usikubali haraka)
Ila we pekee sitaweza kukuacha honey (Nisumbue-sumbue usikubali haraka)
Written by: Fareed Kubanda
instagramSharePathic_arrow_out