Top Songs By Anjella
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Anjella
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Abdu Hamid Said
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Isgilly
Producer
Lyrics
[Verse 1]
Mziki kwangu mi hukuanga ndoto na sikuitimiza kwa kulalaa
Napitia nyingi changamoto yote kuukimbia ufukara
Kipindi naungaunga kwenye soko yan nasongesha miamala
Nikaona tu nijiunge na jeshi ilimradi nami niwe imara aah
[Verse 2]
Jeshi lilifanya nijipindee ilimradi tu na mimi niwe juu
Plan nije kuwa komando jide ama niwe amiri jeshi mkuu
Yalipoanza mambo ya gwaride hapo nikanyosha mikono juu
Kilichofanya yanishinde ni matatizo ya miguu
[Verse 3]
Waliponiacha macho juu na kuninyamazisha mdomoo
Me nina tatizo la miguu wao wakaniunga mkonoo
[PreChorus]
Ntakua mchoyo wa fadhira kwenye maisha yangu nikiacha kushukuru
Maana amani ya moyo wangu naomba Mungu aniangazie nuru
Na nikisema nilikopita njia ilikua mbaya nitakua nakufuru
Huenda Mungu wangu alipanga nipite ili nije kufaulu
[Chorus]
(I feel bless) Bless 'cause God have mercy
Hata kama ulichonacho mie sina mmh
(I feel bless) Bless 'cause God have mercy
[Verse 4]
Me nilishafeli mara kadhaa na maisha mbona yangenishinda
Kama ningekataga tamaa, eh
Acha nisonge mbele kwa hekima
Walosema watasimama nami wamevuta kiti wamekaa ah
[Verse 5]
Kuna muda unapitia simanzi, usiku na mchana
Jitahidi kufanya kazi, ipo siku utasimama
Me nimetokea uswazi, uswahilini sana
Kwetu hakuna ugomvi, ila watu wanapambanaa
[Verse 6]
Kuna muda mapenzi yanaweza kukutoa kwenye reli
Mana kuna wapenzi wanapenda kukuona unavyofeli
Na tatizo la mapenzi, mapenzi yana nguvu kwelikweli
Kwani we hukusikia kuna muwa huko ulizamisha meli eeh
[PreChorus]
Ntakua mchoyo wa fadhira kwenye maisha yangu nikiacha kushukuru
Maana amani ya moyo wangu naomba Mungu aniangazie nuru
Na nikisema nilikopita njia ilikua mbaya nitakua nakufuru
Huenda Mungu wangu alipanga nipite ili nije kufaulu
[Chorus]
(I feel bless) Bless 'cause God have mercy
Hata kama ulichonacho mie sina mmh
(I feel bless) Bless 'cause God have mercy
Written by: Abdu Hamid Said