Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Rapcha
Rapcha
Performer
Cosmas Paul Mfoy
Cosmas Paul Mfoy
Rap
Judith Wambura
Judith Wambura
Lead Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Cosmas Paul Mfoy
Cosmas Paul Mfoy
Songwriter
Judith Wambura
Judith Wambura
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
P Funk Majani
P Funk Majani
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Hebu tazameni, matendo ya Mungu yanavyotisha
Amefanya mengi makubwa ya kustaajabisha
Marafiki leo wana upendo kesho umekwisha
Ila upendo wa Mungu hauwezi kuisha
[Verse 2]
Naamini neno lako linaishi forever
Utandawazi hauwezi kubadili dhambi ikawa haki, never
Umenifikisha sehemu ambazo wala sikuwahi kuzifikiria
Sifa zako nitahadithia
[Verse 3]
Unaniepusha na maadui unanilinda na mabaya
Ambayo hata siyatambui
Mungu uliye hai
Hata mimba zilizotokea kwenye mazingira ya dhambi, watoto umewapa uhai
[Verse 4]
Na kama pumzi unanipa bure
Sasa kivipi tamaa ya pesa initenge na wewe
Nashukuru kwa kunileta hii sayari
Milele nitakuamini Mungu wa kweli, Amen
[Chorus]
Amen Baba, Amen
Upendo wako, huruma yako, Amen
Wema wako, utukufu wako, Amen
Amen Baba, Amen
[Refrain]
Umenipa maarifa, umenipa uhai, umenipa mali
Hata nacho kipaji siwezi sema sijaridhika
Umenipa kile ulichonipa hukunitupa
Nami sitaki juta Baba, nasema Amen
[Verse 5]
Glory to God, utajiri mkubwa ni furaha
Mungu anaweza akubariki mpaka ukashangaa
Niwapo kwenye njaa
Nikumbushe uwa ndege hawalimi, hawavuni ila hawakosi chochote
[Verse 6]
Nilipotoka usiache nikumbusha
Nipe hekima nisitamani magari nisiyoweza kuyaendesha
Niishi kwenye ukweli nidumu
Maana uongo hauishi milele na unaua faster zaidi ya sumu
[Verse 7]
Pia, asante kwa kunipa bidii
Nnapokuomba haujibu haraka unajibu wakati sahihi
Una hekima inayoshangaza dunia
Watu hata tugombane vipi tunashare mvua na jua
[Verse 8]
Nijalie nisilewe sifa
Nikumbuke siku za uhai wangu zinahesabika
Hivyo nikuabudu nikiwa kijana
Nawe utaniweka juu kwa baraka leo zaidi ya jana
[Chorus]
Amen Baba, Amen
Upendo wako, huruma yako, Amen
Wema wako, utukufu wako, Amen
Amen Baba, Amen
Written by: Cosmas Paul Mfoy, Judith Wambura
instagramSharePathic_arrow_out