Lyrics

Mtoto Iddi kazua balaa, kijana Iddi kazua mikosi
Mtoto Iddi kazua balaa, kijana Iddi kazua mikosi
Yupo kama kapandwa na kichaa, anaitaji kurekebishwa
Yupo kama kapandwa na kichaa, anaitaji kurekebishwa
Kuvumilia Iddi anavyofanya, inategemea mtu na mtu
Kabila ama kabila kuna wengine hawana masihala
Watamletea matatizo asijue wapi pa kukimbilia
Watakulea matatizo usijue wapi pa kukimbilia
Iddi zake michapo na pamba za kuazima
Nyumbani ye' huwa hakai anaishi kama kima
Wazazi waliomzaa anawakosea heshima
Akirudi nyumbani Iddi ananukia pombe
Akiulizwa, "Umetoka wapi?" anasema, "Dingi usikonde"
Na kabla ya kuondoka anamkata dingi makonde
Anavyofanya Iddi amerithi kwa baba yake
Sa' kumbe alivyo Iddi baba ivyo sio
Atakuja kukamatwa na kesi za mauaji
Iddi ukimtazama ni mtoto wa makamo
Vibaka wamekamatwa ye' mwenyewe akiwemo
Wamemfikisa kwa baba yake kasema, "Simo"
Wamempiga mapanga kujifanya much know
Anaunguruma na kesi ya kumdhulumu Mr. Joseph Saga
Hivi sasa anatafutwa alilipe lile deni alilokopa kwa bwana John
Ana kesi za wizi zipatazo ishirini na sita
Alivyo na bahati mbaya akikwapua tu wanamshika
Wazazi wake mwenyewe ndio juana na mwinjiga
Amepoteza nafasi ya kuishi kama soldier
Kwani Iddi hawezi kula ugali bila mboga
Kutwa nzima Iddi anakaa kizembe wamemroga
Na tena kunatetezi wanga wamekula kiboga
Wewe Iddi kuwa makini hii tabia haifai
Utapondwa na marungu uone dunia haifai
We nishai, Iddi nishai
Mtoto Iddi kazua balaa, kijana Iddi kazua mikosi
Mtoto Iddi kazua balaa, kijana Iddi kazua mikosi
Yupo kama kapandwa na kichaa, anaitaji kurekebishwa
Yupo kama kapandwa na kichaa, anaitaji kurekebishwa
Kuvumilia Iddi anavyofanya, inategemea mtu na mtu
Kabila ama kabila kuna wengine hawana masihala
Watamletea matatizo asijue wapi pa kukimbilia
Watakulea matatizo usijue wapi pa kukimbilia
Iddi ni kijana mwenye sura ya kibandindu
Iddi ni mtoto wa kwanza wa mzee hamidu
Sema tumseme we' ni kama umemwadhibu
Huyu Iddi ana laana
Iddi kitumwa kwake ni kama umemwonea
Mkimwachia upenyo mnamkuta amepotea
Haoni raha kuishi ye' na yake familia
Anatoka na pombe zake tu akirudi ye' analia
Anamlilia nani na pombe kanywa mwenyewe?
Na huu ni ushauri aliopata kwenye vijiwe
Mzee Hamidu anadharau na kusema, "Lolote liwe"
Alianza tu kidogo ye' kubadili hizi tabia
Kutwa nzima yupo bar anazitiririsha bia
Anasubiri wateja leo ili aweze kuwaibia
'Kamatwa kila wiki watu walishatega njia
Watu wachukia, nini kinachofatia!?
Ni kumponda na kumuua au Mungu kumuokoa huyu Iddi ana laana
Iddi matatani wizi kupenya dirishani
Wala haishi kwa raha amemuibia na Majani
Ye' kila siku kesi tu haziishi mahakamani
Siku tano anautamani
Pita pita kona naona kundi la watu
Wanambeba Iddi kaiba viatu vya watu
Nauliza eti kisa kauza viatu vya watu
Ila mwenyekujua kama Iddi kachukua
Written by: Eva Butiku
instagramSharePathic_arrow_out