Top Songs By Mrisho Mpoto
Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Mrisho Mpoto
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Mrisho Mpoto
Songwriter
Lyrics
(Iye, mjomba, iye)
(Iye, mjomba, iye)
Bora kujenga daraja, kuliko kuta
Chemchem sitemi, ukitaka maji sharti uiname
Bora kujenga daraja, kuliko ukuta
Nikipata nauli, mjini nitakufuata
(Iye, mjomba, iye)
(Iye, mjomba, iye)
Pole sana mjomba
Na kibarua kizito kutaka dunia kuwa kijiji, hongera!
Kile kiitikio cha globalisation kimeimbwa vizuri sana japo hakijakaririwa!
Nasikia wageni wamefurahi sana kusikia sauti yako
Tena wanafurahishwa na ule ubeti wa mwisho uliouongeza
Wa, "Mbio zetu kutoka uhuru mpaka hapa tulipo"
Mjomba, hapa nyumbani tuna hadithi na misemo mingi kujihakiki
Maana lake mtu halimtapishi
Lakini kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga
Juzi walisema kwa kuwa ni wageni kitalani, tukasema tuwape muda
Jana Tumbokali kashikwa na kuku wa jirani
Mkasema imewauma sana, ila bado tuwape muda
Eti kidhibiti cha mwizi wa kuku
Sharti ashikwe na mjuzi au kipande cha mnofu
(Iye, mjomba, iye) ngoma yataka matao jamani!
Mjomba, sina nia nao mbaya, lakini je, unaijua timu yako?
Maana tabia ni kama ngozi ya mwili, hauwezi kuibadili
Na mtoto wa nyoka hafundishwi kuuma
Ukicheka na nyani utavuna mabua mjomba!
Masikini, mtu kwao, ugeni si kitu chema
Msimu wowote kuanza upya si ujinga
Mbwa hafi akiona ufuko
(Iye, mjomba, iye)
Eti wanaomba samahani
Watarudisha uhai wa waliopotea kwa uzembe wao?
Watawanyang'anya waliowapa masikio yetu kama zawadi?
Mjomba, life is not a rehearsal, it is a performance!
Mchelea haki hatendi ukweli, mjomba!
Tazama maisha yetu, utadhani mchezo wa kuigiza
"Migodi sita!," "Yote kwangu"
"Hekali mia moja!," "Najiandaa kustaafu nipate sehemu ya kupumzika"
Mazihala je? Aah, aliyemwoa mtoto wa mjomba wangu, kakake na mamangu nikampa zawadi
Inauma sana!
Inauma sana kugawa malalio yetu kama zawadi, mjomba
Bora kujenga daraja, kuliko kuta
Chemchemi sitemi, ukitaka maji sharti uiname
Bora kujenga daraja, kuliko ukuta
Nikipata nauli, mjini nitakufuata
(Iye, mjomba, iye)
(Iye, mjomba, iye)
Mjomba, tazama kule!
Ile ni shule, na yule anayegawa visheti pale ni mwalimu!
Wengine watauza kesho, wamepeana zamu ya kuyanusuru maisha yao
Japo haipo kwenye mtaala wa shule, tukiona inasaidia tuipitishe
Wala siwachongei, mkiwafukuza, wafukuze wote, majengo tufugie kuku
Labda ndilo tunaloliweza
Eti, "Mchezea zuri, baya umfika", nani kasema?
Wangefanya nini ikiwa hawajui kesho yao?
'Nachojua mimi mjomba, mgomba haushindwi na mkungu
Kwani mkamatwa na ngozi si ndo' mwizi wa ng'ombe?
Vipi mpaka leo wapo? Tena mabingwa wa nahau na methali kule Kitalani
Wana misamiati mipya siku hizi, "Ukijikanyaga tu!" he-eh
Hofu yangu, siwaoni kwenye nyama siku hizi
Hata lile la kulala limepungua, mawili
Wanasoma sana miswada
Au kwa kuwa live runingani wanauza sura
Anyway, tuache hayo, turudi kwenye mada yetu mjomba
Huku kwetu mjomba hali si shwari, kila kukicha, afadhali ya jana
Nadhani! Watu hawajakuelewa
Nikipata nauli nitakuja kukunongoneza mjomba
Please, tafadhali! Acha maagizo mlangoni
Maana siku hizi wanataka sifa kweli, hawachagui pa kupiga
Utasikia, "Lilikuwa likipambana na polisi tukalishinda"
Wapi? Kumbe mpwao na mipango ya kuinusuru nchi
Mpaka zikufikia wewe, huku tia maji, tia maji
Tahamaki, uchaguzi huo, n'natania tu mjomba
Ila kweli nikipata nauli nitakuja
(Iye, mjomba, iye) bora kujenga daraja
(Iye, mjomba, iye) chemchemi sitemi
(Iye, mjomba, iye) bora kujenga daraja
(Iye, mjomba, iye) nikipata nauli
(Iye, mjomba, iye)
(Iye, mjomba, iye)
Written by: Mrisho Mpoto